TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 12 Februari 2016

WAKALIWAO MODERN TARADANCE JUMAMOSI HII NA KILA JUMAMOSI NDANI YA HANAM RESORT KIVULE

NA KAIS MUSSA KAIS.


                 Bendi yako bora ya wakaliwao modern taradance "team masauti" jumamosi hii na kila jumamosi watakuwa wakishusha burudani ya nguvu katika ukumbi wa hanam resort uliopo kivule shule.


                  Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa bendi hiyo thabit abdul alisema kuwa wamejiandaa vyema kabisa kushusha kikosi kizima cha team masauti wakaliwao ili kukonga nyoyo za wadau na mashabiki wa bendi yao, unajua ni muda mrefu sasa tumekuwa tukipokea simu za wapenzi wetu wakituomba kusogeza burudani maeneo ya kwao nasi safari hii tumesikia kilio chao hivyo tunawaomba wajitokeze kwa wingi pasipo kukosa, wasanii waalikwa siku hiyo watakuwa ni msagasumu pamoja nae dogo jack simela wa jagwa musica alisema thabit abdul.


           Wakaliwao modern taradance ni bendi gumzo kwa sasa jijini dar na tanzania kwa ujumla kutokana na kazi zake nzuri ambazo zimekuwa zikifanya vizuri katika media mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni