TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 12 Februari 2016

SWAUMU HARUNA NYOTA YA WAKALI WA TOWN MODERN TAARAB ANAEVUTIWA NA BI MWANAHAWA ALLY!.

NA KAIS MUSSA KAIS.



                Kumekuwa na ongezeko la wasanii wa muziki wa taarab kwa sasa na hii inatokana na wengi kuvutiwa na muziki huu na pia waimbaji wenye majina makubwa kuwa ndio kioo chao katika kuingia kwenye fani hii.


SWAUMU HARUNA MUIMBAJI WA WAKALI WA TOWN.

             Swaumu haruna ni muimbaji chipukizi anaekuja kwa kasi ya ajabu tokea bendi ya wakali wa town modern taarab, muimbaji huyu ambae tayari amesharekodi wimbo mmoja uitwao "rabbi ninusuru na wabaya" amesema kuwa amekuwa akipenda kuimbatoka akiwa mdogo na bila hiyana anawataja wasanii ambao anavutiwa nao na wengine wamemshawishi kwa kiasi kikubwa yeye kujifunza kuimba muziki huu kuwa ni Bi mwanahawa ally, khadija kopa, Isha mashauzi, mwanahawa chipolopolo na mzee yusuph.


          Muimbaji huyu mwenye uchungu wa maendeleo anasema kuwa anawaheshimu waimbaji wote walimtangulia na hata hawa chipukizi wenzie ambao anaweza kusema wapo level moja, unajua ndugu mwandishi sanaa yetu ina miiko mingi sana miongoni mwa miiko hiyo ni heshima kwa wakubwa na wadogo, mimi nimeanzia bendi ya king's modern taarab kwa kijoka ndipo baadae mkurugenzi wangu wa sasa uncle vam au tajiri mtoto aliponiona na kunichukuwa katika bendi yake.


SWAUMU HARUNA AKIWA KWENYE POZI.

        Huyo ndio Swaumu haruna muimbaji mwenye malengo makubwa katika safari yake ya muziki huu wa taarab tanzania, mtandao huu kama ilivyo ada tunapenda kumtia moyo na wala asikatishwe tamaa kwani safari ya muziki ina misukosuko mingi lakini anatakiwa awe jasiri ili kufikia malengo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni