TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 16 Februari 2016

HOMA YA JIJI MODERN TAARAB WAKIWA NA DIRECTOR NDAGE NDAGE WATAMBULISHA NYIMBO MBILI MPYA.

NA KAIS MUSSA KAIS.


               Bendi ya homa ya jiji modern taarab yenye maskani yake mabibo jijini dar es salaam leo hii imetambulisha nyimbo zao mpya mbili kupitia blog hii bora kabisa ya ubuyu wa taarab.


WAIMBAJI WA HOMA YA JIJI WAKIWAJIBIKA STEJINI.

             Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa bendi hiyo mbaraka albela ambae pia ni mtunzi wa mashairi wa siku nyingi alisema kuwa wameamua kuja katika soko la ushindani na wamejipanga vyema kukabiliana na lolote lile! unajua ndugu mwandishi, mimi taarab naijua vyema na wala sio mgeni katika tasnia hii, mimi nilikuwepo pale dar modern taarab na nimetunga nyimbo nyingi sana pale, baadae niliamua kuelekea victoria modern taarab, lakini sasa nimekuja na kitu changu mwenyewe homa ya jiji moder taarab, kwahiyo wadau wajiandae kupata vitu vizuri toka kwetu.


WAIMBAJI WA HOMA YA JIJI MODERN TAARAB.

           Akizitaja nyimbo hizo mbili ambazo wamezitambulisha leo alisema, wimbo wa kwanza unaitwa "maneno ya kuambiwa" huu kaimba bibie Raya nassor na wimbo wa pili unaitwa "mtakalia hayo hayo" huu kaimba bibie Azza mohamedy ambae ni mlemavu wa macho yaani haoni kabisa ila sisi tumempa nafasi na kaimba vizuri sana, vile vile nyimbo zote mbili kinanda amepiga director ndage ndage mtaalam asie chuja alimalizia kwa kusema!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni