TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 13 Februari 2016

UBUYU WA TAARAB TUNATOA POLE KWA ISHA MASHAUZI NA FAMILIA NZIMA KWA KUONDOKEWA NA MZEE WAO.

NA KAIS MUSSA KAIS.


               Mtandao wa ubuyu wa taarab sambamba na dawati zima la habari la blog hii tunapenda kutoa pole zetu kwa mkurugenzi wa mashauzi classic Isha mashauzi kwa kuondokewa na baba yake mzazi mzee Ramadhan wa makongo.

ISHA MASHAUZI.


             Tunatambua wazi kuwa kwa sasa Isha mashauzi yupo katika wakati mgumu ila sisi mtandao wa ubuyu wa taarab tunapenda kumtia nguvu na kumuahidi kuwa nae bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu kwake kwani kila kilichopewa pumzi na mwenyezimungu kitakufa, mzee wetu ametangulia ila nasi tupo njiani kwani hatujui siku wala saa, pole sana Bi rukia juma mke wa marehemu, pole isha mashauzi na pia pole kwa saida mashauzi bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihidimiwe!.


         Taratibu za mazishi zinafanywa ili kuuhifanyi mwili wa mpendwa wetu mzee ramadhan wa makongo, sisi tulimpenda ila mwenyezimungu kampenda zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni