Malkia wa mipasho tanzania bibie khadija omary kopa, jana tarehe 5/5/2016 aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kwenda katika kituo cha watoto yatima cha mtambani kilichopo maeneo ya magomeni makuti
na kutoa misaada mbalimbali pamoja na kula nao chakula cha mchana.
KHADIJA OMARY KOPA AKIKATA KEKI YAKE MAALUM. |
Katika ziara hiyo khadija kopa alisindikizwa na wasanii wake sambamba na wadau nikimaanisha "team ogopa kopa", akizungumza na mtandao huu khadija kopa alisema kwamba amepatwa na hali ya kwenda kwa watoto yatima kulingana na maisha ambayo wanaishi watoto wale, mwenyezimungu hakuwaonea ila sisi tulio vyema ni wajibu wetu kuwasaidia wenzetu wenye matatizo kwani hata vitabu vyetu vya dini vinasema hivyo.
WASANII, TEAM OGOPA KOPA NA WATOTO WA KITUO, HAPA WAKIWA NA KHADIJA KOPA. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni