TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 6 Mei 2016

JAHAZI MODERN TAARAB, WAKALIWAO,YAMOTO BENDI NA MSAGASUMU KUSINDIKIZA UZINDUZI WA OGOPA KOPA JUMAMOSI YA LEO!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


            Hatimae ile siku maalum kwa uzinduzi wa bendi ya ogopa kopa na sambamba na albam mpya imewadia ni leo pale katika ukumbi wa kisasa wa dar live.


           wakizungumza na mtandao huu kwa nyakati tofauti viongozi wa bendi hizo wamejisifia kila mmoja kufanya vizuri zaidi ya mwenzie, akiongea kwa niaba ya jahazi modern taarab mkurugenzi mipango wa bendi ya jahazi. Hamisi boha amesema sisi kama ada tutakamua mwanzo mwisho ndani ya ukumbi huo wa dar live, vile vile tutachukuwa nafasi hiyo kuwatangaza rasmi waimbaji wetu wapya aisha othman vuvuzela na zubeda mlamali hivyo wapenzi naomba mje kwa wingi kuwasapoti waimbaji hawa.


         Nae meneja ally juma wa wakaliwao modern taradance amesema amejiandaa vya kutosha kwa kuwaletea raha kutoka kwa wasanii wangu wa wakaliwao, nae dogo asley amesema walikuwa kambini kuandaa mambo mazito yote ni kwa ajili ya uzinduzi wa mama yetu khadija omary kopa. nimeomba wakati kama huu ili kuzamia moja kwa moja...msagasumu amesema siku hiyo ataimba nyimbo zake zote ambazo ziliwahi kutamba.


         Leo kwa pamoja tuungane ili kuleta mabadiliko katika tasnia hii ya taarab nchini tanzania, dawati zima la habari la ubuyu wa taarab litakuwepo dar live ili kurekodi matukio kadhaa, njoo ubudike kwani kuna nini tena?,.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni