TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 7 Mei 2016

JAHAZI MODERN TAARAB NDANI YA TRAVETINE HOTEL MAGOMENI JUMAPILI YA LEO...UNAANZAJE KUKOSA?.

NA KAIS MUSSA KAIS.


MFALME MZEE YUSUPH, LEYLA RASHID NA KHADIJA YUSUPH WAIMBAJI WA JAHAZI.

          Bendi yako bora ya jahazi modern taarab wana wa nakshinakshi chini ya mfalme mzee yusuph, leo jumapili watakuwa katika uwanja wao wa nyumbani travetine hotel magomeni kuanzia saa mbili usiku.


         Siku hii ya leo itakuwa na ma-surprise kibao na burudani zote zitapigwa yaani zile za zamani na hata hizi mpya za sasa, mkurugenzi wa mipango wa bendi hiyo hamisi boha amesema kuwa jahazi ni bendi kubwa isiyofananishwa na bendi yoyote kwa ubora hapa tanzania, waimbaji wake ni wale wenye viwango na hata wapiga vyombo wanajitambua.


        Siku ya leo kutakuwa na wageni waimbaji kutoka zanzibar ambao watapewa nafasi ya kuimba japo sio rasmi ila ni ndugu zetu sana, pia hadija yusuph na leyla rashid ambao hawakuwepo katika show iliyopita, leo hii watakuwepo hivyo wale mashabiki ambao hawakuridhika kwa kutokuja kwa wasanii hawa wiki iliyopita basi wasiwe na shaka kwani leo jumapili watakuwepo ndani ya nyumba. mwisho aliwaomba wadau na wapenzi kujitokeza kwa wingi leo pale travetine hotel magomeni jijini dar es salaam kupata raha na wala sio karaha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni