TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 8 Mei 2016

FATMA MUSSA MUSSA:- SINA MPANGO WA KUIHAMA DAR MODERN TAARAB, HAPA NIMEFIKA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


FATMA MUSSA MUSSA MUIMBAJI WA DAR MODERN TAARAB.

              Unapoamua kwenda kuona show za dar modern taarab pale katika ukumbi wao wa kisasa magomeni basi utakutana na sura tulivu isiyo na makuu iliyopambwa na tabasamu la nguvu toka kwa fatma mussa mussa muimbaji mwenye kipaji kikubwa sana.


         Mtandao huu ulipata habari za chini ya kapeti kwamba kuna bendi inamnyemelea muimbaji huyu ili aweze kujiunga nao ndipo tulipofanya jitihada za kumtafuta ili aweze kuthibitisha taarifa hizi je ni kweli? au ni maneno ya walimwengu tu!. kwanza fatma alianza kwa kushangaa taarifa hizo na kusema sio kweli na wala sina mpango wa kuihama dar modern taarab, mkurugenzi wangu Alhaji abdallah feresh anatuthamini sana sisi wasanii, sasa sehemu kama hii nahama alafu niende wapi?, sina mpango huo wala sitarajii.


        Fatma mussa ni muimbaji asie na makuu, nidhamu yake katika muziki huu ndio silaha yake ya mafanikio akiwa na dar modern taarab, nafikili hapo fatma amekomesha uvumi usio na msingi juu yake, hana mpango wa kuihama bendi yake ya dar modern taarab na wala hatarajii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni