TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 9 Mei 2016

MUSSA BESI AU "BABA WARDA" APATA AJALI YA PIKIPIKI MAENEO YA TAZARA JIJINI DAR.

NA KAIS MUSSA KAIS.


            Mpiga gitaa la besi wa bendi ya jahazi modern taarab,mussa besi au baba warda kama anavyotambulika na wengi siku ya jumatano tarehe 4/5/2016 alipata ajali ya pikipiki maeneo ya tazara wakati akielekea katika show ya jahazi modern taarab kiwalani.


MUSSA BESI AKIWA NA GONGO BAADA YA KUTOKA HOSPITALI.

          Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mussa alisema kwamba ilikuwa ni mida mida ya saa mbili usiku baada ya kuona nimechelewa na tunapiga show mbali siku hiyo ya jumatano nilimpigia simu kijana ambae nimempa pikipiki yangu aendeshe kama bodaboda, kwamba anifuate maeneo ya temeke nilipokuwepo na anipeleke kazini huko kiwalani nae alikuja, wakati tupo katika pikipiki pale maeneo ya kona ya tazara kama unaelekea uwanja wa ndege kuna gari ikawa inakuja kwa nyuma yetu ilipotufikia ikatugonga na kurushwa upande wa pili wa barabara.


HAPA AKIONEKANA MWENYE SURA YA HUZUNI KUBWA.

       Bahati nzuri hakukuwa na gari iliyokuwa inakuja, ila kulikuwa na lori limepaki pembeni basi tulivyorushwa ule upande wa pili yule mwenzangu akaingia hadi chini ya uvungu wa gari ila kwa upande wangu niliishia nje, yule mwenzangu akapoteza fahamu pale pale na damu zikawa zinamtoka mdomoni na puani, ila mimi kwa muda ule nilijiona nipo sawa, nikanyanyuka na kuifuata pikipiki. Bahati nzuri nilimuona mtu ambae tunafahamiana nae pale pale katika ajali nikamuachia ile pikipiki yangu nami na yule mwenzangu kwa msaada wa wasamalia wema tukapakizwa katika bajaji kuelekea hospitalini kwa matibabu, lakini kwanza tulipitia polisi tukapata PF3 ndipo tukaenda hosptali amana ilala.


HAPA NI BAADA YA KUZUNGUMZA NA MWANDISHI WA HABARI HIZI.

     Tulipofika mwenzangu akawekewa dripu nami nikapelekwa kushonwa maana mguu umechimbika sana nahisi lami ndio imenichimba sana mguuni, hivyo nimeshonwa nyuzi tisa kwa nyama ya ndani ya mguu na nyuzi nane kwa nyama ya nje ya mguu, pia nimeshonwa nyuzi mbili mkononi vile vile nimechubuka sana juu ya jicho lakini huku sijashonwa namshukuru mungu. kwa sasa naendelea vizuri na siku ya alhamisi nimeambiwa na daktari niende hospitali nikatoe nyuzi na kuona maendeleo ya kidonda. Mtandao wa ubuyu wa taarab unampa pole mussa besi na ndugu yake kwa ajali hiyo iliyo wakuta lakini tunaamini mwenyezimungu atawasimamia na watapata nafuu mapema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni