TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 11 Julai 2017

QUEEN SALMA:- SIYALIPIZI MABAYA NI WIMBO WANGU MPYA WENYE KISA HALISI KILICHONIKUTA.

Na pambe za taarab.

    Muimbaji tegemezi wa supershine modern taarab Queen Salma amezungumza na mtandao huu wa pambe za taarab juu ya ujio mpya wa wimbo wake uliopewa jina la "siyalipizi mabaya" kuwa ni kisa cha kweli kilichonikuta ndani ya familia yangu.

      Queen Salma alisema kuwa niliamua kukaa chini na kutunga wimbo huo baada ya kufikwa na mitihani na ndani ya familia yangu mwenyewe, walimwengu wanasema tenda wema uende zako kweli sasa nimeamini alisema Queen Salma.

    Naomba mwenyezimungu anijaalie niweze kurekodi wimbo huo ili niweze kifikisha hisia zangu kwa jamii kwani naamini wapo watu ambao nao wamefanyiwa kama nilivyofanyiwa mimi na familia alimaliza kwa kusema.

      Queen Salma ni muimbaji nyota ambae aliwahi kutamba na nyimbo kadhaa kama kiokote, huna style, usia wa baba na mola kaninyooshea hizi zote ameziimba akiwa na bendi ya supershine modern taarab yenye makazi yake magomeni jijini dar.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni