TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 12 Julai 2017

SABAHA SALUM MUCHACHO, NYOTA ISIYOCHUJA KATIKA MUZIKI WA TAARAB AFRIKA MASHARIKI.

Na pambe za taarab.

   Fimbo ya mungu, huu ni wimbo ambao niliwahi kushuhudia harusi moja hapa jijini dar, ndugu wakiparurana kwa ujumbe mzito uliopo humo haswa kwa yule mlengwa ambae hakutendewa haki.

    Huyu ndie Sabaha salum muchacho mwana mama ambae nampenda kupita kiasi kutokana na tungo zake na uimbaji wake usio na papara!. Sabaha salum muchacho ni muimbaji alieifanyia makubwa sana taarab hapa nchini na africa kwa ujumla! kwa sasa mama huyu anafanya biashara zake mwenyewe hapa jijini dar isipokuwa kunapotokea mialiko kadhaa ya bendi haswa melody na Zanzibar stars basi unaweza kumuona huko, pia katika harusi mbalimbali hupatikana kwa maelewano maalum.

    Nilipata bahati ya kukutana nae na kumuuliza vipi taarab kwa sasa unaionaje?, kwa upole alinijibu taarab inapotea, taarab haina mtetezi, taarab inayumba hakuna jipya katika taarab kwa sasa!, enzi zetu tunaimba taarab ilikuwa na heshima kuanzia uimbaji mpaka katika mavazi lakini leo hii mtu anakuja kuimba taarab amevaa suruali? alihoji Sabaha!.

    Sidhani kama taarab inaweza kurudi ikawa kama zamani sifikirii, maana hakuna mbinu mbadala za kuinusuru taarab kila mmoja anavutia kwake bila kufikiria nini kinakuja kutokea mbele alisema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni