TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 9 Julai 2017

VITUO KADHAA VYA REDIO NCHINI VYAPUNGUZA MUDA WA HEWANI KWA VIPINDI VYA TAARAB.

Na pambe za taarab.

      Muziki wa taarab nchini Tanzania umekuwa ukipoteza umaarufu wake kwa kadri siku zinavyosonga mbele mpaka kupelekea vituo kadhaa vya redio nchini kufuta kabisa vipindi hivyo na zingine kupunguza muda wa hewani wa vipindi hivyo.

      Hili limeonekana kwa redio kadhaa na sababu kubwa ni kukosekana kwa wadhamini katika kuendesha vipindi hivyo hewani, kuna baadhi ya redio mfano TBC fm wameondoa kabisa kipindi cha taarab kilichokuwa kikirushwa kuanzia saa 3 kamili asubuhi, redio king's njombe wameondoa kabisa kipindi cha taarab, redio time's fm ya dar imepunguza muda wa hewani wa kipindi chake cha taarab ambacho zamani kilikuwa kinaanza saa sita mchana mpaka saa kumi jioni, lakini kwa sasa kinaanza saa sita mchana mpaka saa tisa alasiri.

   Hii ni baadhi ya mifano kwa redio kadhaa hapa nchini, kikubwa kinachopelekea khali hii ni kukosekana kwa wadhamini wa kusapoti vipindi hivyo redioni. Hebu tujiulize kwa pamoja ni nini sababu inayopelekea khali hii kutokea?, kipindi haswa kinachoishusha taarab?, maswali ni mengi sana yanaweza kuzalishwa hapa.

     Mtandao huu unapenda kuwakumbisha viongozi wa muziki huu kuamka huko walipolala na kujitoa vibanzi machoni mwao kwani jahazi linazama taratibu na hakuna wa wakuliinua, huu ni muziki wenye asili ya mwafrika miongoni mwa miziki hiyo, leo hii inakuwaje watu wanashindwa kukaa na kutafakari hiki kinachokwenda kutokea?...AMKENI SASA!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni