Na pambe za taarab.
Malkia wa mipasho nchini tanzania khadija omary kopa anakuja na kitu kipya kabisa kilichopewa jina la "wigi linawasha" chini ya utunzi wake young hassan ally "mzee wa ngenga".
Akizungumza na mtandao huu mtunzi wa wimbo huo young hassan ally alisema ameamua kumtungia shairi hilo Bi khadija kopa ili awape fundisho mawifi wote wasiojielewa, maana kwa sasa imekuwa too much! kwa mawifi kuwaonea choyo wake za kaka zao.
Humo khadija kopa amechamba haswa na kutoa funzo ni jinsi gani mawifi wanatakiwa wawe!. Mdau mmoja wa taarab nchini baada ya kusikia kuwa malkia khadija kopa anakuja na kitu hicho alipiga hodi ofisini kwetu ili japo apatiwe mashairi kabla ya kuusikia wimbo wenyewe lakini alipopigiwa simu Hassan ally alisema huyo mdau awe na subira kwani mara nyingi jambo jema linahitaji subira.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni