Na pambe za taarab
Ebony fm kutoka nyanda za juu kusini mkoani iringa ni redio inayokuja kwa kasi hapa jijini dar na inapatikana 106.9 fm, mtangazaji maarufu zaidi kwa hapa dar tokea redio hiyo ni Tinner turner ambae anaongoza kipindi cha taarab.
Alhamisi iliyopita alikuwa ni mgeni katika group la pambe za taarab whatsap na alikutana na maswali kadhaa wa kadhaa toka kwa wadau na wanachama wa group hilo. Miongoni mwa maswali aliyoulizwa ni kuwa kwanini anapokuwa akitangaza huwa anamuiga sana Hatya omary mtangazaji wa redio one ambae hapo kabla aliwahi kupitia redio hiyo ya ebony fm nakutangaza pia.
Akijibu swali hilo Tinner alisema kiukweli katika mind yangu sikuwahi kufikilia kufanya hicho kitu na wala haitotokea, mimi natangaza kwa uwezo wangu na kipaji alichonijaalia mwenyezimungu wala sijawahi kuiga na wala sifikirii, vile vile wakati mimi naingia ebony fm Hatya omary sikumkuta alikuwa ameshaondoka redio one nami nilitokea mkoani mtwara katika redio moja kule. Naheshimu sana uwezo wa Hatya na namheshimu kama mtangazaji mwenzangu lakini kusema kwamba namuiga yeye katika utangazaji wangu hilo nakataa kabisa alisema Tinner.
Wadau wengi wamekuwa wakimhusisha Tinner na baadhi ya watangazaji, wengine wakisema kuwa sometimes anatangaza kama Geah habibu, mara anachamba kama Dida wa times fm na wengineo, sisi kama pambe za taarab tunapenda kumuambia Tinner kwamba ukishaanza kuona watu wanakufananisha na flani jua wazi tayari umekubalika kikubwa ni kukomaa na kusonga mbele ili uje ufikie malengo yako...big up! sana kwa kazi nzuri "malkia wa nyanda za juu kusini" Tinner Turner wa ukweli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni