Na pambe za taarab.
Ile segment ambayo imeendelea kujichukulia umaarufu katika tasnia ya taarab nchini "sindano za motto" jana ili m'bamba khanifa maulid jike la chui na aliulizwa maswali mengi sana ikiwemo kujielezea historia yake na mengineyo.
Khanifa aliingia katika group milango ya saa moja na dakika 3 usiku na moja kwa moja wanachama na wadau wa group hilo walianza kwa maswali, miongoni mwa maswali ambayo alikutana nayo ni hili:- Je khanifa maulid mpaka sasa unazungumza na Isha mashauzi? na kama hamzungumzi unafikiri kwanini...je kuna juhudi zozote ambazo zimewahi kufanyika ili muweze kuzungumza tena kama zamani?...hilo ndilo swali ambalo naweza kusema lilimbandanisha khanifa na jasho lilimtoka!.
Akijibu swali hilo khanifa maulid alisema, mimi kwa sasa sina mawasiliano ya aina yoyote yale na Isha mashauzi na naona sawa tu sababu sina ambacho nimepungukiwa, kuna kipindi Dida wa times fm alijitahidi sana kutaka kutupatanisha lakini alishindwa, kwa upande wangu sikuwa na tatizo la kuzungumza na yeye Isha nilikuwa tayari lakini mwenzangu alikataa na hakuonekana kama analihitaji hilo kwahiyo ilishindikana kihivyo, kwa sasa kila mmoja na hamsini zake na maisha yanaendelea siwezi kulazimisha kuzungumza na mtu ambae hayupo tayari alimalizia kujibu khanifa maulid.
Mtandao huu unapenda kuchukuwa nafasi hii kuwaasa wale wote ambao wamekoseana kwamba ni vyema wakayazungumza yakaisha maana maisha yenyewe ni mafupi na chuki hasama hazifai katika jamii, Isha na khanifa kaeni chini muyamalize si vyema kuiendekeza hali hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni