Na pambe za taarab.
Muimbaji chipukizi ambae anafanya vizuri kwa sasa katika bendi ya Jahazi modern taarab khadija mbegu yupo katika kuwindwa na bendi mbili kubwa za taarab nchini na hii ni kutokana na uwezo wake mkubwa alionao pindi anapokuwa stejini.
Bendi hizo mbili ambazo zote zinapiga muziki wa "gate collection" kiingilio pesa!, kwa nyakati tofauti zimeonekana zikimsaka khadija mbegu bila mafanikio na hii ni kuhofia viongozi wa Jahazi wasije wakawashitukia. Unajua kwa sasa yule msichana anafanya vizuri sana naamini kama nitampata bendi yangu itakuwa imepata kifaa cha nguvu mno, tatizo lililopo mwenyewe anaonekana ana mapenzi makubwa sana na bendi hii ya jahazi modern taarab, sio kama siwaoni wengine hapana ila uwezo wa kuimba na kucheza kwa msichana huyu ndio ushawishi mkubwa kwangu...namuhitaji sana kiukweli alisikika kiongozi huyo.
Mtandao huu unazijua bendi hizo ila ni mapema sana kuzitaja kwa sasa, tulimtafuta khadija mbegu mwenyewe na kumuuliza je tayari amepata taarifa hizi za yeye kutakiwa na bendi mbili kubwa? Na khadija alijibu kuwa hana taarifa hizo ndio kwanza anasikia, na hata kama hizo bendi zitamfuata jibu lake ni kwamba hana mpango wa kuihama jahazi modern taarab sababu kwanza ana mapenzi ya dhati na bendi hii na vile vile hana tabia ya kuhamahama bendi. Napenda niwatoe wasiwasi viongozi wangu, wasanii wenzangu na mashabiki wa jahazi kwamba sina mpango wa kuhama na wala sitarajii kamwe...mimi ni jahazi damu alimaliza kusema huku akicheka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni