TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 8 Agosti 2017

TINNER TURNER:- TOKEA EBONY FM, SIOGOPI DUDU WALA MENDE NA MANENO YANGU SIO UMA KUSEMA UTALIA CHAKULA.....

Na pambe za taarab.

Katika ile segment ya mjue mtangazaji wako, alhamisi ya wiki hii tutakuwa na Tinner turner mtangazaji toka ebony fm iliyopo iringa tanzania akijibu maswali ya wanachama wa group la pambe za taarab whatsap ambao walimteua ajiunge nao tayari kwa baadhi ya maswali ambayo wangependa kujua toka kwake.

Tinner mtoto wa kimara anaefanya vizuri nyanda za juu kusini, siku hiyo atawekwa mtu kati na wanachama hao kwani wana kiu haswa yakumswalika maana wamekuwa wakimsikia tu akiporomosha madongo na wengine wamefika mbali zaidi kwa kusema alipaswa kupata redio hapa dar ili aende sambamba na mtangazaji wa kituo cha redio cha times fm Dida kwani maneno yao yanaendana sana!, mbona patachimbika bila jembe siku hiyo ya alhamisi! alisikika mdau mmoja wa group hilo akuzungumza kwa voice note.

Mjue mtangazaji wako ni moja wapo ya segment ambazo zipo katika group la whatsap la pambe za taarab ambalo limedhamilia kidhati kabisa kuutetea muziki huu ingawa wapo baadhi ya wadau wamekata tamaa na kuufananisha muziki huu na dansi jinsi ulivyopotea kabisa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni