TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 7 Agosti 2017

SAADA NASSOR:- SIJAWAHI KUTENGENEZA FILAMU ZA X, HUO NI UZUSHI NA UZANDIKI.

Na pambe za taarab.

Saada nassor kwa sasa ndie malkia wa taarab kwa zanzibar, vile vile anaongoza kwa kupata tuzo nyingi kutokana na utendaji wake mzuri wa kazi alionao. Kwa sasa Saada ni muimbaji wa Island superstar wajelajela original bendi inayomilikiwa na jeshi la mafunzo zanzibar.

Siku ya jumatatu alikuwa ndie mgeni katika group la whatsap la pambe za taarab kupitia segment ya sindano za motto ambayo huanza saa moja kamili usiku mpaka saa mbili kamili usiku, kwanza Saada alianza kwa kuelezea historia yake kimuziki na baadhi ya changamoto ambazo amekutana nazo mpaka sasa ndipo baadae maswali yakaanza kuulizwa, aliulizwa maswali mengi sana lakini kutokana na nafasi tumeamua kuchukua maswali mawili tu muhimu ambayo aliyajibu na kuwaletea humu wale ambao hawapo katika group lile.

Swali la kwanza aliulizwa je una mpango gani wa kufanya kazi na director Thabit abdul? nae Saada alijibu hiyo ni ndoto niliyonayo na inshallah kwa uwezo wa mungu naamini ipo siku Thabit abdul atanitengenezea wimbo na utakuwa moto balaah!, vile vile nina ndoto ya kufanya kazi na Diamond platinum bila kumsahau Hammer Q hawa wasanii nawafeel sana wanajua kiukweli nitafurahi sana kama siku moja ndoto yangu itatimia.

Swali la Pili aliulizwa kuna kipindi zilizagaa video zinazokuonyesha ukiwa katika tukio la aibu yaani ukifanya sinema ya X na mwanaume iliyosemekana alikuwa ni mumeo je ni kweli?, Saada alijibu kuwa sikweli na hata siku moja siwezi kufanya uchafu kama ule, mimi ni mtoto wa kislam mwenye maadili haswa ya dini naanzaje kufanya mambo kama yale machafu...unajua watu au mtu akiamua kukutengenezea kashfa basi anaweza na utashindwa kumchukulia hatua sababu humjui utampatia wapi, ile kashfa iliniumiza sana na nashukuru mashabiki zangu wameelewa ukweli na wananipenda maradufu yake! huyo ambae alinitengenezea kashfa ile kamwe sitomsahau maishani ila mungu pekee ndie ajuae...ninachoweza kusema ni kwamba zile habari sio kweli na ndio sababu niliimba ule wimbo "mmeshayasema kimeniathiri nini?" Maalum kwa hao waliotegemea ningeporomoka kimuziki kumbe ndio kwanza trip za ulaya kila kukicha nazipata! mungu sio athuman wala Jafary tusijisahau alimaliza kwa kusema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni