MAKALA MAALUM.
Na pambe za taarab.
Kuna ule msemo wa kiswahili usemao "ulie okota nae kuni ndio wakuota nae motto" hapa wahenga walikuwa na maana kubwa sana, ukiuchunguza kwa makini msemo huu utapata maana na utang'amua jambo la hekima sana!.
Katika siku za hivi karibuni kumezuka vikao vinavyofanyika kisirisiri ambavyo nia na madhumuni yake ni kufanya mageuzi katika uongozi wa jahazi ulio madarakani na kuurudisha ule uongozi wa zamani...hili sio baya kufanyika kama mkurugenzi mkuu anaona mwenendo wa viongozi wake wa chini haupo sawa! anaweza kuongeza nguvu ili kunusuru bendi kutetereka. Lakini huwezi kufanya vikao vya siri pasipo kuwa shirikisha wale uliowapa dhamana ya kuongoza, hapa utakuwa huwatendei haki na utakuwa umewadharau sana zaidi ya sana!, binadamu kukosea ni kawaida na kama unahisi hawapo sawa unaweza kuwaita na kufanya nao kikao cha kuwakumbusha ni nini wanatakiwa kufanya ili bendi ipate mafanikio.
Mtandao huu wa pambe za taarab upo katika kuuinua muziki huu kwahiyo linapokuja suala la kuudidimiza muziki huu kamwe hatuwezi kuufumbia macho ni lazima tuseme ingawa inaweza kuonekana baadhi ya viongozi watachukia kwa hiki kilichoandikwa lakini habari ndio hiyo. Kwa sasa ndani ya bendi ya jahazi modern taarab kumezuka sintofahamu kati ya mkurugenzi mkuu na viongozi wake wa chini, uchunguzi wa kina uliofanywa na mtandao huu na kujiridhisha unaonyesha mkurugenzi ameanza vikao na baadhi ya viongozi ambao walimsaliti na kumkimbia na kumuacha dhalili huku wakitoa kashfa kubwa kwamba jahazi limezama na hakuna wakuliinua tena, watu wamepata shida, wameishi maisha ya tabu kwa kujinyima ili jahazi lisimame na kweli mwenyezimungu kajaalia jahazi kwa sasa limesimama na wanafanya show mara nne kwa wiki, leo hii mkurugenzi anataka kuwaondoa wale aliopata nao shida na kuwarudisha wale wasaliti...hii haiko sawa!, ndio pale niliposema "ulie okota nae kuni, ndio wakuota nae motto".
Mkurugenzi kabla haujaanza kufanya chochote katika hayo uliyoyadhamilia napenda nikueleze yafuatayo, kwanza viongozi ambao umeplan kuwaondoa nafsi zao zimekunja kifupi hawajaridhika na unachotaka kufanya, pili kumbuka nguvu zao walizopoteza katika kupigania bendi isimame, wametoa nguvu zao, wametoa muda wao, wametoa pesa zao na vitu vingine si uungwana kuwaengua kwa dharau kiasi hicho!, hao unaowakumbatia sasa kumbuka ndio waliokukimbia na kukupa maneno mengi ya dharau na kashfa...leo hii umesahau?, Jahazi mpaka hapo ilipofikia sio kwa uwezo wako binafsi, mawazo yenu kwa pamoja katika vikao vyenu vya uongozi ndio vimeifikisha hapo jahazi mpaka hao wengine wanatamani kurudi...hebu kaa na ufikilie mara mbili upo sahihi kwa unachotaka kufanya au?...Geuka nyuma na kumbuka ulipotoka na unapoelekea naamini utagundua tatizo...Alamsiki!.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni