TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 5 Agosti 2017

THABIT ABDUL:- KHADIJA YUSUPH BADO NI MKURUGENZI WA WAKALIWAO, ANAETANGAZA AMEACHA BENDI ANAJISUMBUA.

Na pambe za taarab.

Mkurugenzi mtendaji wa wakaliwao modern taradance Thabit abdul "director" ameibuka na kukanusha taarifa zilizozagaa kwa wadau kwamba khadija yusuph amehama bendi ya wakaliwao kutokana na kutoelewana na baadhi ya viongozi wenzake!.

Akifanya mahojiano na mtandao huu Thabit alisema nashangazwa na taarifa zinazozagaa katika magazeti mbalimbali kwamba khadija yusuph ameacha bendi ya wakaliwao...nashindwa kuelewa, kwanza napenda niwaambie watanzania kuwa khadija yusuph ni mmoja wa wakurugenzi wa bendi hii na tuna makubaliano ya kimkataba baina yake na yangu sasa leo itashangaza kuona mkurugenzi anaamua kuiacha bendi yake mwenyewe ni ajabu!.

Unajua naweza kusema kuna baadhi ya wandishi wanatumiwa kuihujumu wakaliwao lakini nawaambia wazi wanajisumbua watamaliza wino katika peni zao kwa kuandika taarifa zisizo na ukweli wowote!, mwandishi unashindwa kubalance stori! hata sheria za uandishi hazisemi hivyo kabisa, ndio pale ninaposema kuna baadhi wanatumiwa kuichafua wakaliwao lakini kwa uwezo wa mungu watashindwa alisema mkurugenzi huyo.

Napenda niondoe wasiwasi wapenzi na mashabiki wa wakaliwao kwamba khadija yusuph bado yupo wakaliwao na ataendelea kuwa wakaliwao, kukosekana kwa baadhi ya show ni kwasababu ya matatizo ya kifamilia tu na wala si vinginevyo alimaliza kwa kusema. Katika siku za karibuni khadija yusuph alihusishwa na kuiacha bendi ya wakaliwao jambo lililopelekea baadhi ya magazeti kuandika habari hizo. Tusubiri tuone ni kweli anayo yasema Thabit abdul au taarifa zinazoripotiwa na vyombo vya habari kuwa khadija ameiacha wakaliwao ni za kweli?...TUSUBIRI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni