Na pambe za taarab.
Mtangazaji wa kipindi cha ng'aring'ari kinachorushwa na cloud's televisheni Sakina lyoka jana aliwathibitishia wadau na wapenzi wake kuwa hana ugomvi na mtangazaji mwenzie wa cloud's redio Geah habibu kama ambavyo watu wamekuwa wakivumisha.
Akijibu maswali kwa kujiamini, utulivu na uelewa mkubwa Sakina alitupiwa swali hilo na mdau aitwae Oddo Hawa tokea tanga kwamba kipindi cha nyuma ilivuma sana kwamba Sakina lyoka hana maelewano mazuri na Geah habibu na chanzo cha tatizo hilo ikasemwa ni kugombea kipindi ndani ya cloud's media. Sakina kwa kujiamini alikanusha taarifa hizo na kusema wapo sawa kabisa na Geah habibu na hakuna tatizo lolote lile.
Unajua sisi yaani mimi na Geah habibu sote ni wanadamu tuna mapungufu yetu kwahiyo inawezekana huko nyuma ilitokea labda tukakwaruzana lakini kila mmoja alijua tatizo lipo wapi na kumaliza tofauti na maisha yanaendelea, Geah habibu ni mfanyakazi mwenzangu ambae pia tunawasiliana sana tukiwa kazini na hata tukiwa mbalimbali tunawasiliana pia, so napenda nikanushe uvumi huo sio kweli bali mimi na Geah habibu tupo poa sana tu na ni mshikaji wangu alimaliza kwa kusema Sakina lyoka.
Mamaa wa dawa yao alikuwa akihojiwa na wadau, wapenzi, wasanii na watangazaji ndani ya group la whatsap liitwalo pambe za taarab "wadau" katika ile segment iitwayo mjue mtangazaji wako ambayo huwa hewani kila siku ya alhamisi kuanzia saa moja kamili usiku mpaka saa mbili kamili usiku. Mtandao wa pambe za taarab upo katika kuuinua na kuukuza muziki huu ambao katika siku za karibuni umeonekana kupoteza dira.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni