TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 3 Agosti 2017

JUMANNE ULAYA, REKODI YAKE YA MILLION 6 NA GARI NDOGO KUELEKEA T MOTTO HAIJAVUNJWA MPAKA LEO!.

Na pambe za taarab.

Jumanne ulaya ni mpiga gita la sollo wa bendi ya jahazi modern taarab ambae ana makubwa mengi aliyoyafanya katika tasnia ya taarab nchini.

Wakati anaanza kuingia katika muziki huu walio wengi walimchukulia ni mtu wa kawaida sana ambae hawezi kuleta madhara wala kusumbua katika tasnia hii lakini makucha yake yalianza kuonekana wakati yupo east african melody pale alipopiga sollo flani lenye mahadhi ya tabora mkoani kwao lenye style ya kabango kama lile ambalo alikuwa akipiga shem kalenga. Wakati Jumanne ulaya anaingia katika muziki wa taarab alikuta kuna mpiga sollo maarufu ambae alikuwa anapewa heshima ya aina yake nae si mwingine isipokuwa ni Abdallah bwigabwiga.

Pamoja na changamoto kubwa alizokutana nazo wakati anaanza kujiingiza katika muziki huu lakini Jumanne ulaya hakukata tamaa alipambana zaidi, Jina lake haswa lilianza kujulikana pale alipojiunga na jahazi modern taarab enzi ya mzee yusuph na kupewa cheo cha u-director. Kuna siku moja wakati jahazi inafanya show katika kiwanja chake cha nyumbani yaani travertine  magomeni mke wa mzee yusuph yaani leylah rashid alichelewa kufika stejini basi J4 bila kujari huyu ni mke wa mkurugenzi wake alimrudisha nyumbani kwa kuchelewa kwake huko kufika kazini, huyo ndio jumanne ulaya mwenyeji wa tabora.

J4 anapokuwa kazini huwa serious hataki mchezo kabisa na ndio sifa kuu ya mnyamwezi huyu, ni yeye ndio msanii ambae anashikilia rekodi kubwa ya kununuliwa kwa shilingi million 6 na gari ndogo aina ya Carina kutoka jahazi na kwenda T motto hakuna msanii yeyote ambae amewahi kupata pesa kama hizo katika taarab mpaka sasa. Unapomuuliza je unakumbuka mpaka sasa umesharekodi nyimbo ngapi jibu atakuambia ni zaidi ya mia moja na kuendelea zingine hata sizikumbuki ukiniambia nizitaje kwa majina. Kwa sasa jumanne ulaya yupo katika bendi yake ya zamani ya jahazi modern taarab na hii ni baada ya kuachana na ogopa kopa classic bendi inayomilikiwa na malkia wa mipasho nchini khadija omary kopa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni