TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 2 Agosti 2017

MUIMBAJI SAADA NASSOR, KUWEKWA MTU KATI JUMATATU IJAYO NDANI YA SINDANO ZA MOTTO!.

Na pambe za taarab.

Muimbaji bora wa taarab visiwani unguja, Saada nassor kutokea kundi la highlanders superstar wajelajela original siku ya jumatatu ijayo atakuwa katika segment ya "sindano za motto" kwenye group la whatsap la pambe za taarab.

Akizungumza kwa njia ya simu kutokea visiwani humo Saada alisema nimefarijika sana kwa mimi kuteuliwa kufanya interview kwenye group hilo bora zaidi kwa sasa kwani humo nitaweza kukutana na watu mbalimbali kutoka mikoa tofauti mpaka nje ya nchi, mimi naamini pasipo wao siwezi kuwa Saada Nassor hususani katika suala zima la burudani nawategemea sana wao kwani sapoti zao ndio zimenifikisha hapa nilipo alizungumza Saada.

Saada aliteuliwa na wanachama wa group hilo kuwepo katika segment hiyo wiki ijayo maana wana mengi ambayo wanataka kujua toka kwake, Saada ndio msanii anaeshikilia ile tuzo ya muimbaji bora katika modern taarab zanzibar kwa sasa, hivyo basi wasomaji wa blog hii tunawaahidi kuwaletea mahojiano kamili ambayo yatafanyika kwenye group hilo siku hiyo ya jumatatu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni