TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 2 Agosti 2017

SAKINA LYOKA WA CLOUD'S TV, USO KWA MACHO NA WADAU WA PAMBE ZA TAARAB KESHO SAA MOJA USIKU USIKOSE.....

Na pambe za taarab.

Ile segment inayokuja kwa kasi ya ajabu ki-umaarufu hapa mjini "mjue mtangazaji wako" kesho alhamisi majira ya saa moja za usiku itaendelea na safari hii mgeni mwalikwa ni bibie sakina lyoka Mamaa wa dawa yao tokea clouds televisheni atahojiwa na wadau, mashabiki, watangazaji mbalimbali na wasanii kadhaa ambao wanapatikana katika group hilo la whatsap linalokwenda kwa jina Pambe za taarab.

Sakina lyoka alithibitisha kuwepo katika segment hiyo na kutuma voice note ambayo imewahakikishia wanachama wa group hilo kwamba sakina atakuwepo kikubwa ni kujiandaa kwa maswali kama ambavyo imekuwa ikifanywa pindi mgeni anapoingia humo. Mtangazaji wa citizen redio ya nchini kenya baada ya kusikia sauti ya sakina lyoka akizungumza kuwa atakuwepo alifurahi sana na kusema kuwa kuanzia sasa anaingia mitandaoni ku-google maswali ya kumuuliza sakina pindi atakapoingia kesho.

Huu ni utaratibu ambao viongozi wa group hilo la pambe za taarab whatsap wamejiwekea kuita watu wanaohusika kwa kiasi kikubwa katika group na kuulizwa maswali, ukiondoa segment hiyo lakini pia kila jumatatu kuna segment ingine ambayo inaitwa sindano za motto hapa msanii wa taarab huwa anahusika kwa maswali toka kwa wanachama wa group hilo, tungoje tuone nini ambacho sakina ataulizwa hapo kesho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni