TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 2 Agosti 2017

NAIMA MOHAMEDY AJIUNGA NA JAHAZI MODERN TAARAB HUKU AKILI YAKE IKIWA OGOPA KOPA!!.

Na pambe za taarab.

Muimbaji wa kutegemewa wa ogopa kopa Naima mohamedy amejiunga na jahazi modern taarab huku akili yake ikiwa ndani ya bendi yake hiyo ya zamani.

Unaweza kushangaa ndugu msomaji kwanini iwe hivi lakini ukweli ni kwamba Naima mohamedy aliomba kwenda kuimba jahazi modern taarab kama "ndo ndo" na viongozi wa ogopa kopa walimruhusu kwa roho moja, lakini kama ujuavyo wahenga wanasema "asali haionywi mara mbili", baada ya kukaa kwa muda ndani ya jahazi modern taarab Naima ameamua kutorudi tena ogopa kopa kwakuwa bendi yake hiyo ya zamani haina show za muendelezo kama jahazi ambao wana show kuanzia alhamisi mpaka jumapili.

Jumapili iliyopita Naima alisikika akihojiwa na geah habibu ndani ya clouds fm na kukiri kuwa kwa sasa yeye ni msanii wa jahazi modern taarab na amehama rasmi bendi ya ogopa kopa jambo lililopelekea viongozi wa ogopa kopa kuanza kuhaha kumtafuta Naima ili awaeleze ni kweli haswa amehama bendi yao? lakini baada ya kupigiwa simu na viongozi hao Naima alisema yeye bado ni mali ya ogopa kopa na sio jahazi. Mtandao huu kama ilivyo kawaida yake tulimtafuta kiongozi wa jahazi modern taarab Prince amigo na kumuuliza je ni kweli Naima ni msanii wao? nae alijibu kuwa ni kweli kwa sasa Naima ni msanii wa jahazi modern taarab ila kwa taarifa zaidi nionane na mkurugenzi mkuu ambae ni Hamisi Boha ndio anaelewa zaidi.

Hatukuishia hapo tulimtafuta Naima mohamedy mwenyewe azungumzie hili na yeye alisema ni kweli kwa sasa yeye ni msanii wa Jahazi modern taarab na sio ogopa kopa tena isipokuwa katika ile show kubwa inayotarajiwa kufanyika pale dar live Naima atamsaidia khadija kopa katika chorus lakini yeye ni msanii halali wa jahazi kwa sasa na hayo ndio maamuzi yake sababu muziki ni kipaji chake na anaishi na familia inayomtegemea. Mwisho kabisa alisisitiza kuwa anaomba maamuzi yake yaheshimiwe, hilo ndilo sakata la Naima na jahazi pamoja na ogopa kopa tusubiri tuone nini kitatokea hapo mbele.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni