TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 1 Agosti 2017

KHADIJA KOPA AKILI KUWA HANA MAZUNGUMZO NA HANIFA MAULIDI...WALA NAMBA YAKE YA SIMU KWA SASA HANA!.

Na pambe za taarab.

Malkia wa mipasho nchini tanzania ambae pia ni mkurugenzi wa ogopa kopa classic bendi Bi khadija omary kopa amekili kuwa kwa sasa hana mahusiano ya karibu na khanifa maulidi "jike la chui" aliewahi kuwa msanii wake ndani ya ogopa kopa.

Khadija kopa aliyasema hayo jana katika group la whatsap la wadau, wasanii na watangazaji liitwalo pambe za taarab wakati akifanyiwa mahojiano ndani ya segment iitwayo  "sindano za motto" ambayo huwa ni kila jumatatu saa moja kamili mpaka saa mbili kamili, hapo huwekwa kiti motto wasanii ambao hupendekezwa waingizwe humo kwa mahojiano.

Akijibu swali la mmoja wa wadau, malkia huyo alisema kuwa kwa sasa mimi na khanifa hatuna mawasiliano kabisa, kwanza hata namba yake ya simu sina labda ningeweza kumpigia, kuna kipindi huwa natamani sana kuwasiliana nae lakini nashindwa kwakuwa namba yake ya simu sinayo. Mimi na khanifa hatujagombana imetokea tu kwahiyo kumkumbuka ni kitu cha kawaida kwa mtu ambae ulizoeana nae! lakini naamini ipo siku moja tutakutana hata barabarani na tutasalimiana kwani mimi sina tatizo alizungumza malkia huyo kwa sauti ya unyonge sana.

Khadija kopa na khanifa maulidi ikumbukwe walikuwa wakiitana mtu na wifi mwenzie wakati wapo pamoja ogopa kopa...sasa uwifi huo ulitokea wapi? ni wao wenyewe ndio wanajua jambo la umuhimu hapa ni kuwaombea kwa mungu wawili hawa ili waweze kuzungumza kwa uhuru kama zamani kwani mwenyezimungu huwa anazichukia nafsi zenye visasi pamoja na magomvi yasiyo kwisha ndio maana vitabu vya dini vimeandika samehe saba mara sabini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni