TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 31 Julai 2017

PRINCE AMIGO, NYOTA MWENYE MALENGO MAKUBWA NA JAHAZI MODERN TAARAB.

Na pambe za taarab.

Unapolitaja jina la Prince amigo katika tasnia hii ya taarab, basi ujue umetaja jina kubwa sana ambalo litakuja kufanya vizuri sana zaidi ya sana, huyu ni mfalme mpya wa taarab kwa sasa na pia ni msanii kiongozi wa bendi ya Jahazi modern taarab.

Alipoanza kuingia katika muziki huu hakuna alietegemea kama anaweza kuwa kama alivyo sasa, naamini ni yeye mwenyewe ndio ambae alikuwa na kiu ya kufika mbali zaidi na kwa juhudi zake na watu waliomzunguka ameweza kufika alipopataka ingawa mwenyewe anasema bado ana safari ndefu zaidi ya mafanikio. Amigo ni msanii mwenye msimamo na asieyumbishwa na tamaa ndogo ndogo kwa kulithibitisha hili ni pale bendi ya jahazi modern taarab ilipoyumba na kuondokewa na wasanii karibia asilimia 95% lakini yeye alibaki na kusema atahakikisha bendi inarejea na kweli amefanikiwa ingawa haikuwa rahisi.

Ukipata nafasi ya kwenda katika onyesho lolote la jahazi modern taarab utafurahi na roho yako pale anapopanda prince amigo stejini kwani huwa hashuki mpaka awe ameimba nyimbo zaidi ya tatu na zaidi, hii inathibitisha kwamba Amigo ni mapafu ya mbwa ana uwezo mkubwa kwani huwa anaimba na kucheza kwa stepu akishirikiana na wacheza show wake, katika muziki huu wa taarab hakuna muimbaji yeyote wakiume ambae ana style kama ya Prince amigo.

Prince amigo sio msanii mwenye kujisikia, kwa kifupi yeye hajui kulinga kama wengine, nilipata bahati ya kuwahoji watangazaji wa vipindi vya taarab katika redio kama watatu hivi wakiwemo Gea habibu wa clouds na Dida shaibu wa times fm na wote kwa wakati tofauti walisema kuwa prince amigo ni msanii wa mfano kwani muda wowote ukimuhitaji kwa interview hana tatizo kabisa na kwa style hii ya kutokulinga basi atafika mbali sana kupita alivyokuwa mzee yusuph.

Huyo ndie Prince amigo, nyota wetu wa leo muimbaji kiongozi wa jahazi modern taarab, kwa sasa amigo anaandaa wimbo mpya ambao atatoka nao ndani ya jahazi hii mpya, wadau, wapenzi na mashabiki wa muziki wa taarab jiandaeni kupata kitu kipya kabisa toka kwa prince amigo siku chache zijazo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni