TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 30 Julai 2017

UONGOZI WA OGOPA KOPA WAKANUSHA TETESI ZA KUTIMKA KWA WAIMBAJI WAKE WATATU.

Na pambe za taarab.

Kufuatia taarifa zilizotolewa jana na mtandao huu kuhusu wasanii watatu wa ogopa kopa kutimka, leo hii uongozi wa bendi hii umeibuka na kukanusha tetesi hizo.

Akizungumza na mtandao huu katibu wa bendi hiyo ambae pia ni muimbaji Prince black kopa mtoto wa malkia wa mipasho nchini alisema kuwa tetesi hizo sio kweli isipokuwa kilichopo hapo ni kwamba wasanii hao wanakwenda kuimba huko kama "ndondo" tu lakini ogopa kopa tukiwa na show zetu basi tunajumuika nao kama kawaida.

Unajua bendi yetu ya ogopa kopa huwa hatuwazuwii wasanii kwenda kuimba popote pale ikiwa kama sisi hatuna show na hii huwa inawasaidia wenyewe kuwaingizia kipato ukizingatia khali ya uchumi ni mbaya kwa kipindi hiki. Hivyo napenda kuwatoa wasiwasi wapenzi na wadau wetu kuwa wasanii hao ambao wanawaona huko wakiimba bado wapo ogopa kopa na huko wameenda kwa ruhusa ya uongozi mzima wa bendi yetu alimaliza kwa kusema.

  Tuliwaahidi wasomaji wetu kuwa tutawaletea mrejesho wa tetesi hizi na kweli tumetimiza na kauli ya uongozi wa ogopa kopa ndio hiyo na inapaswa iheshimiwe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni