Na pambe za taarab
Kile kilio kikubwa kilichokuwa kikisumbua wadau na wapenzi wa taarab nchini kimepata dawa, baada ya mtandao wa pambe za taarab whatsap kuanzisha segment iitwayo "kijamvi cha motto" ambayo itakuwa hewani kila siku ya jumapili saa moja kamili mpaka tatu kamili za usiku.
Hapa wadau mbalimbali watakuwa wakihojiwa na kutoa yao ya moyoni juu maisha yao na mustakabali mzima wa muziki huu wa taarab, kitakachokuwa kinafanyika ni mdau mmoja wapo kuingizwa katika group hilo la whatsap au kama ni mwanachama na yupo humo, basi anatakiwa kujirekodi voice note na kujielezea historia yake kiufupi, ni faida gani amepata mpaka sasa tokea aingie katika udau, ushauri gani anaowapa wahusika wa muziki huu, hasara ambazo amepata kutokana na yeye kuwa mdau na mengineyo mengi. Baada ya hapo wadau wenzie watasikiliza voice note hiyo ndipo maswali yataanza rasmi toka kwao.
Katika siku inayofuata mahojiano hayo yatachapishwa katika blog hii ili wale ambao sio wanachama wa group hili la whatsap wapate kuelewa ni baadhi gani ya maswali aliulizwa mdau huyo, hapa haangaliwi huyu mdau superstar au huyu mdau mchanga, wote ni sawa na wanastahili haki kwa kila mmoja, hivyo basi tunaomba ushirikiano wenu wa dhati wadau katika kufanikisha kipengele hiki kilichowekwa maalum kwa ajili yenu...Ahsanteni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni