Na pambe za taarab
Enzi za uhai wa nyawana isale fundikira walikuwa wakiitana pacha kati yake na Queen salma muimbaji kiongozi wa bendi ya supershine modern taarab yenye makazi yake magomeni jijini dar.
Mtandao huu ulipata bahati ya kumtembelea Queen salma nyumbani kwake magomeni na kupiga nae stori mbili tatu kuhusu tasnia hii ya muziki wa taarab na bendi yake ya supershine. Mtandao huu ulitaka kujua toka kwake ni kwanini mpaka sasa hajaimba wimbo alioachiwa kama urithi na Pacha wake marehemu Nyawana usemao "sikosi wa kunizika", Queen alianza kwa kusema nashindwa kuimba wimbo ule sababu nimeshajaribu na nimeshindwa sababu nyawana kwangu alikuwa ni mtu muhimu sana na alikuwa ni zaidi ya rafiki...nilikuwa namchukulia kama ndugu yangu wa damu maana mambo mengi tumefanya pamoja kiukweli siwezi kila nikijaribu nalia machozi tu namuomba huko aliopo anisamehe maana nimemshiba sana pacha wangu nampenda na nitaendelea kumpenda daima milele.
Akiendelea Queen salma alisema najitahidi kumfanyia visomo vya mara kwa mara ili mwenyezimungu ampunguzie adhabu za kaburi, sote njia yetu moja na yeye ametangulia tu naamini siku moja nitaonana tena na pacha wangu, mungu ampe kauli thabiti alimaliza kwa kusema huku akijifuta machozi.
Marehemu Nyawana isale fundikira alifariki tarehe 11 mwezi wa 11 mwaka 2013 na kuzikwa kwao tabora tarehe 13 mwezi wa 11 mwaka 2013 katika makaburi ya machifu huko kijijini itetemiya, ameacha watoto wawili wakike na wakiume. Kabla hajafariki nyawana alikuwa ameolewa na kais mussa kais mdau na kiongozi wa muziki huu wa taarab. Mungu amrehemu na ampe kivuli miongoni mwa vivuli vya peponi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni