Na pambe za taarab.
Mpambano wa bendi tatu Jahazi modern taarab, Yah tmk modern taarab na wakaliwao modern taradance uliofanyika jana jumapili katika ukumbi wa travertine magomeni ulimng'arisha chipukizi wa jahazi modern taarab khadija mbegu khali iliyomchanganya fatma mcharuko na kupanda steji kumtunza wakati akiimba wimbo wa maruperupe!.
Khadija ambae ukipata bahati ya kumuona unaweza kumdharau na kumuona wa kawaida lakini ana ni msichana aliejaaliwa kipaji kikubwa cha kuimba na mwenyezimungu. Wakati anatangazwa kwenda kuimba wimbo wa maruperupe khadija alionekana kujiamini kupita kiasi na alipokamata kipaza sauti mashabiki walilipuka kwa shangwe na mayowe huku wakisema kuwa mrithi wa fatma mcharuko ameshapatikana! baada ya muda kidogo kupita huku watu wakicheza kwa furaha ndipo fatma mcharuko mwenyewe alipopanda stejini na kwenda kumtunza pesa.
Mtandao huu ulipata bahati ya kuzungumza na fatma mcharuko na kumuuliza anamzungumziaje khadija mbegu muimbaji ambae anakuja kwa kasi ya sunami kwa sasa!, alianza kwa kusema kuwa khadija ni muimbaji mzuri tena sana, huyu ni hazina ya Jahazi modern taarab kwa sasa, amenichanganya mpaka nikapanda stejini kwenda kumtunza kwajinsi alivyokuwa akiimba vizuri, namuomba khadija mbegu anitafute nimuongezee maujuzi zaidi na kumuonyesha njia ambazo mimi nimepita mpaka hapa nilipo, uzuri ni kwamba khadija tunafahamiana na ni mtu ambae ukimuelekeza jambo akubali kubadilika alimaliza kwa kusema fatma mcharuko.
Mtandao huu kwanza kabisa unampongeza fatma mcharuko kwa kukubali uwezo wa msanii mchanga kama khadija mbegu na kukubali kumuelekeza ili aweze kufikia malengo kama ambavyo yeye amefikia, pili tunapongeza khadija mbegu kwa kuendelea kufanya vizuri kila kukicha katika tasnia hii ya muziki wa taarab nchini tanzania kikubwa tunamuomba asilewe sifa akaze buti maana safari yake kimuziki bado ni ndefu sana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni