TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 11 Septemba 2017

BLACK KOPA AAMUA KUACHANA RASMI NA MUZIKI WA TAARAB, SABABU KUBWA NI.........

Na pambe za taarab.

Mtoto wa malkia wa mipasho nchini tanzania prince black kopa leo majira ya saa sita za mchana alipiga simu katika ofisi zetu na kuzungumza kuwa ameamua kuachana rasmi na kuimba muziki wa taarab na kujitoa kabisa katika bendi inayomilikiwa na mama yake mzazi ya ogopa kopa classic bendi.

Akizungumza kwa msisitizo mtoto huyo wa malkia alisema kuwa amechoshwa na braa! braa! zisizokwisha toka kwa uongozi wa bendi hiyo ya ogopa kopa na taarab kwa ujumla!, viongozi wa ogopa kopa hawapo serious na kazi, sasa mimi kamwe siwezi kukaa katika kitu ambacho hakipigi hatua kwenda mbele, nimeamua kuacha mwenyewe kwa ridhaa yangu wala sijashawishiwa na mtu ila nitabakia katika project ya zile nyimbo za marehemu kaka yangu Omary kopa pamoja na studio yangu ya kurekodi muziki na video...taarab tena mimi basi.

Mtandao huu ulifanya jitihada za kumtafuta mama mzazi wa black kopa ambae ni malkia wa mipasho nchini bibie khadija omary kopa, lakini mpaka tunakwenda mitamboni simu yake ilikuwa haipatukani, tunawaahidi wasomaji wetu kwamba tutawaletea sehemu ya pili ya sakata hili na sasa itakuwa ni kupata maelezo toka kwa mama mzazi wa kijana huyu je anachukuliaje uamuzi uliofanywa na kijana wake na vipi kuhusu hizi tuhuma kwamba viongozi wa ogopa kopa hawapo makini katika utendaji wao khali inayopelekea baadhi ya wasanii kuwalalamikia, ikumbukwe kuwa hata Naima mohamedy nae aliwahi kusema kuwa uongozi wa ogopa kopa umekaa tu wala hawatafuti show huku wakijua wazi kwamba wasanii waliowengi hawana kazi mbadala wanategemea muziki ndipo maisha yao yaweze kwenda. Naima aliwahi kuwa anaenda jahazi modern taarab kuimba ndondo, tusubiri tuone viongozi wa ogopa kopa watalitoleaje ufafanuzi suala hili.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni