TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 13 Septemba 2017

WASANII WATATU WAKIKE CHIPUKIZI WANAOFANYA VIZURI KATIKA MUZIKI WA TAARAB KWA SASA!.

Na Pambe za taarab

Wasanii chipukizi ambao wanafanya vizuri katika bendi mbalimbali za taarab hapa nchini tanzania wapo wengi sana lakini tasmini hii ni kwa niaba ya mtandao huu wa pambe za taarab na si vinginevyo.

1. Khadija mbegu:- wa jahazi modern taarab yeye anashika namba moja kwa umahili wake katika uimbaji na hata kulimiliki jukwaa!, huyu kwa historia fupi hana muda mrefu ndani ya tasnia hii sababu anasema alianza wakaliwao ingawa kipindi alipokwenda wakaliwao alikuwa ni mwanafunzi zaidi, alipotoka hapo akaingia kolombwe modern taarab na hatimae akaingia jahazi modern taarab ambapo yupo mpaka sasa!, khadija ni msichana mwenye kipaji kikubwa sana ingawa bado hajapata bahati ya kurekodi lakini ni msanii tegemeo pale jahazi pamoja na uchipukizi alionao hapo.

2. Mwajuma kidoti:- huyu anashika namba mbili kwa wasanii chipukizi, mpaka sasa amefanikiwa kurekodi wimbo wake mmoja uitwao mbaya hana alama chini ya director senior bachelor pale ndani ya bendi ya majaz modern taarab, khadija amezunguka bendi kadhaa za chimi hapo nyuma lakini jina lake limekuja kung'aa zaidi ndani ya bendi ya majaz modern taarab.

3.Baby ruby:- ni muimbaji wa kutegemewa wa supershine modern taarab yenye maskani yake magomeni jijini dar, huyu ni msanii chipukizi ambae anakuja kwa kasi kubwa kwa ustadi wake wa uimbaji na ubora wa sauti aliojaaliwa. Baby ruby kabla hajaingia supershine alikuwa katika bendi ya lunch time ya manzese na pia alifanya vizuri sana pale.

Hao ndio wasanii watatu bora chipukizi ambao wanafanya vizuri kwa sasa katika bendi zao kwa muda huu, hii ni kwa niaba ya mtandao wa pambe za taarab kwahiyo hata wewe kwa nafasi yako unaweza kuchagua wasanii wako bora na wanaofanya vizuri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni