Na pambe za taarab.
Aisha othman vuvuzella muimbaji wa kutegemewa wa yah tmk modern taarab, alikana taarifa ambazo zilisambaa kipindi cha nyuma na kumsababishia kuandamwa sana na wadau wasio elewa kwamba yeye ndie ambae alikuwa akifanya mbinu za wazi wazi kibibi yahya aondoke wakaliwao.
Vuvuzella alikuwa akijibu maswali ya wadau mbalimbali ndani ya group la whatsap "pambe za taarab" ndani ya segment iitwayo sindano za motto ambayo inakuwa hewani kila jumatatu saa moja kamili usiku mpaka mbili kamili, mmoja wa wadau alimuuliza vuvuzella kwamba kuna kipindi habari zilisambaa kuwa wewe upo na mipango ya kumuhamisha kibibi yahya wakaliwao na kumpeleka jahazi je zilikuwa na ukweli wowote habari zile?, kwanza vuvuzella alikataa kuzungumzia jambo lile lakini baada ya wadau kumsihi sana wanahitaji kusikia toka kwake ndipo alipokubali na alianza kwa kusema.
Katika khali ya kawaida mimi vuvuzella sijakuwa wakala wa wasanii kwanza kazi hiyo hainifai na siitaki kabisa, kibibi ni rafiki yangu na alinifuata kama rafiki na kunieleza dhamira yake nami kama rafiki yangu nikajaribu kumtafutia nafasi pale jahazi kipindi kile au pale mashauzi, lakini Sikutegemea kwamba mambo yanaweza kuwa mazito kama ilivyokuja kutokea. Ni kweli niliongea na mzee yusuph pamoja na kiongozi mmoja wa mashauzi ambae sipendi kumtaja jina na wote walikubali kumchukuwa kibibi ila kabla mambo hayo kuendelea ndipo taarifa ziliwafikia akina Thabit abdul na tatizo kubwa kutokea...sitaki kuzungumzia sana issue ile sababu yameshapita nami tunazungumza vizuri na kibibi pamoja na huyo Thabit abdul nashukuru...ila kiukweli khali ilichafuka kipindi kile alimaliza kwa kusema.
Jumatatu ya wiki ijayo ndani ya segment hiyo ya sindano za motto tutakuwa na black kopa kama mgeni ambae atahojiwa, miongoni mwa maswali yatakayo tawala ni kwanini ukeachana na ogopa kopa blend inayomilikiwa na mama yako mzazi?...jambo gani likekufanya utangaze kuacha muziki wa taarab, tusubilie tuone nini kitakachojiri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni