Na pambe za taarab.
Khali ya sintofahamu katika ndoa ya Mwinyimkuu na Maina thadei imezua utata baada ya kuzagaa taarifa kwamba wawili hao kwa sasa hawapo tena ndoani!, habari hii iliyoshtua wapenzi na wadau wa muziki wa taarab ilipofika katika dawati la habari la mtandao huu ulianza kufanya juhudi za kuwatafuta wana ndoa hawa ambao kwa sasa wanaishi zanzibar.
Tulianza kwa kuzungumza na Maina thadei ambae kwanza alipoambiwa kuwa habari zao zimefika katika mtandao wetu alishtuka sana!, lakini kwa upande wake Maina alisema ni kweli kwa sasa wana matatizo na mume wake ambayo yamepelekea kutozungumza na kuishi mbalimbali lakini mpaka sasa bado hajapewa talaka ina maana ni wanandoa!, unajua ndugu mwandishi, mimi mara nyingi huwa sipendi kuweka hadharani mambo yangu binafsi hivyo sina la zaidi ktk kukueleza hili na sipo tayari kumpa mtu kiki bila ya sababu ya msingi alimaliza kwa kusema.
Tulipomtafuta Mwinyimkuu ili nae aseme chochote juu ya issue hii, alisema:- Maina bado mke wangu mpaka sasa na wala hatuna tatizo lolote lile na kama unasema Maina amesema sisi tuna matatizo ktk ndoa yetu basi hilo mimi silijui ninavyofahamu tupo sawa tu!, alipoulizwa imekuwaje ukafuta picha zote ambazo unaonekana upo beneti na Maina ktk account zako zote mitandaoni? alisema huu ni uamuzi tu na yeyote anaweza kufanya hivyo kama ana picha nyingi ambazo ameplan kuziweka tena ndivyo pia ilivyo kwangu mimi. Watu wanaongea sana juu yetu lakini niwaambie tu kama itafikia sisi kuachana basi tutaweka wazi tu wala haina shida ndugu mwandishi alimaliza kwa kusema Mwinyimkuu.
Mtandao huu haukuridhika na majibu ya wawili hao ndipo alipotafutwa rafiki wa karibu wa wawili hawa ambae wanaishi nae huko zanzibar na kumuuliza juu ya issue hii nae alianza kuzungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake! hawa jamaa kwa sasa sio mke na mume tena kwa kifupi wameshaachana kabisa kwa talaka isipokuwa wenyewe wanaficha ila Maina yupo kivyake na Mwinyimkuu yupo kivyake ndoa imeshavunjika kabisa. Mwinyimkuu na Maina thadei ni wasanii wa muziki huu wa taarab ambao walioana na kuvuta hisia za wadau, wapenzi na mashabiki wa tasnia hii ambao walikuwa wakiwapenda sana! kwa sasa wawili hao wamehamishia shughuli zao visiwani zanzibar, Mwinyimkuu akiwa katika bendi ya wajelajela ambapo inasemekana anatoka kimapenzi na muimbaji machachari Husna Hassan chitoto nae Maina anafanya show katika mahotel mbalimbali ya kitalii visiwani humo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni