Na pambe za taarab.
Lile sakata la Mwinyimkuu na Maina thadei limeingia sehemu ya pili baada ya muimbaji wa bendi ya magereza wana wa jelajela ya zanzibar Husna hassan almaarufu "chitoto" kuhusishwa kwamba yupo katika mapenzi mazito na Mwinyimkuu khali iliyopelekea ndoa ya Mwinyimkuu na Maina thadei kuingia ktk mgogoro mkubwa ambao umeleta mpasuko baina yao kama si kuachana kama inavyovumishwa!.
Mtandao huu wa pambe za taarab kama kawaida yake baada ya kupata fununu hizo ulimtafuta kwa njia ya simu Husna hassan "chitoto' muimbaji machachari wa magereza ambae anafanya vizuri sana kwa sasa visiwani zanzibar ili kutaka kujua juu ya tetesi hizi na shutuma dhidi yake je ni kweli?, kwa upande wake Husna alikana taarifa hizo na kushangaa kuwa zinatoka wapi?, unajua ndugu mwandishi huyu Mwinyimkuu ni msanii wa magereza kwa sasa na sisi ndio ambao tumempokea kama wenyeji wake! Mwinyimkuu amekuwa akicheka na kila mmoja pale kazini na hakuna kati yetu ambae ana mahusiano ya kimapenzi na Mwinyimkuu.
Kama Mwinyimkuu kweli ana matatizo na mkewe basi mimi sio sababu labda wenyewe wana tofauti zao, nijuavyo mimi tupo katika project ya Mwinyimkuu na wimbo wake mpya uitwao sweet of my heart na mimi mule nimecheza kama video Queen, sasa labda zile picha ambazo tumepiga na Mwinyimkuu tukiwa location ndio zinawapa watu kisebusebu! ila zile ni picha tu na ule ni wimbo wa mapenzi hivyo unapocheza ni lazima uonyeshe hisia alisema Chitoto.
Tulimuuliza mbona inasemekana wewe umeachana na mumeo na unataka Mwinyimkuu achukue nafasi? Husna alicheka sana akasema kuachana ni jambo la kawaida katika mapenzi...ameachwa Winnie Mandela first lady itakuwa mimi!, hiyo sio sababu ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mwinyimkuu, naomba ieleweke kuwa Mwinyimkuu ni msanii mwenzangu tu pale wajelajela na wala si vinginevyo alimaliza kwa kusema Husna.
Sintofahamu ya jambo hili bado inaendelea na wahusika wote wamekuwa wazito kuweka wazi jambo hili, hebu wasomaji wetu endeleeni kuvuta subira naamini mwisho wa siku kila jambo litakuwa wazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni