TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 5 Oktoba 2017

BABY RUBY AJIUNGA RASMI NA YAH TMK MODERN TAARAB.

Na pambe za taarab.

Aliekuwa muimbaji wa bendi ya supershine modern taarab Baby ruby jana jumatano rasmi ndani ya ukumbi wa dar live mbagala alianza kazi katika bendi yake mpya Yah tmk modern taarab inayoongozwa na mkubwa fellah.

Akizungumza na mtandao huu Baby ruby alisema kuwa nimeamua kuondoka supershine na kujiunga na yah tmk ili kupata changamoto zaidi katika kazi, na pili nina kiu ya kurekodi wimbo mpya sababu wakati nipo pale supershine sikuwahi kupata nafasi ya kurekodi. Naomba wadau na mashabiki wa yah tmk wanipokee kwa moyo mmoja na sapoti yao ni jambo la muhimu sana kwangu alimaliza kwa kusema.

Nae mkurugenzi wa bendi hiyo ya yah tmk said fellah Akizungumza na mtandao huu alisema yupo ktk kuiboresha zaidi bendi yake na uwezo wa Baby ruby ndio uliowashawishi viongozi wenzangu kufanya mazungumzo nae na kumchukuwa kabisa katika bendi yetu! hapa tutampatia wimbo mpya na stahiki zake kadhaa atatimiziwa sababu ni muimbaji mzuri.

   Bendi ya yah tmk inafanya show zake ktk ukumbi wa dar live kila siku ya jumatano na siku ya jumamosi huwa wanafanya show zao ktk ukumbi wa buliyaga temeke jijini dar nyote mnakaribishwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni