Na pambe za taarab.
Muimbaji wa kutegemewa wa yah tmk modern taarab Omary tego a.k.a. mgodi unao tembea amezungumza katika group la whatsap la wadau juu ya uwepo wa coast modern taarab na yah tmk modern taarab.
Akifafanua zaidi baada ya kuulizwa swali amekuwa akijigawa vipi wakati inapotokea bendi zote mbili zinakuwa na show kwa siku moja?, Tego alisema hilo ni jambo rahisi sababu mimi najua wazi yah tmk ni bendi ambayo imeniajiri na coast ni bendi ya nyumbani yaani ya familia hivyo nitaelekea kule kwenye ajira yangu yaani yah tmk na kuacha coast ikiendelea na show maana wapo vijana pale wakiongozwa na mdogo wangu yusuph tego mkono wa london.
Unajua watu wamekuwa wakitafuta sababu ili ionekane kama naijari sana coast kuliko yah tmk, naomba wale wasioelewa ni vyema wakanitafuta mwenyewe nikawajuza maana mimi nashirikiana vyema na wandishi kuliko kuandika mambo yasiyo na ukweli wowote ambao utapelekea uvinjifu wa amani na maelewano. Nimefurahi kuulizwa swali hili humu kwani naamini waliokuwa hawajui watajua sasa kupitia hapa alimaliza kwa kusema Omary tego.
Mtandao huu una group la whatsap la wadau, wasanii pamoja na watangazaji ambapo humo kuna segment mbalimbali ambazo zinaendeshwa maalum kwa wadau, watangazaji na wasanii pia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni