Na pambe za taarab.
Muimbaji machachari anaekuja kwa kasi ya tsunami OG-MAIGI ameibuka na wimbo matata wenye miondoko ya singeli akimshirikisha msanii nguli wimbo uitwao "SUBIRA".
Msanii huyo ambae kwa sasa yupo chini ya kampuni ya skillman media inayoongozwa na mkurugenzi kais mussa kais au Rais wa mbagala amesema kuwa miongoni vya vibao vyake vizuri na ambavyo amekuwa akipata comment nyingi za pongezi basi ni wimbo huu wa Subira, hivyo anawaomba wadau na mashabiki kumpa sapoti kubwa ili aweze kufanya mambo makubwa zaidi katika siku za usoni. Nae mkurugenzi kais mussa kais akizungumza kwa niaba ya kampuni yake alisema ameamua kumsaidia OG-MAIGI kwakuwa ameona juhudi binafsi toka kwa msanii huyo na anaamini mwenyezimungu akipenda watafika mbali sana.
Wimbo huo wa subira ambao kwa sasa unapatikana katika stesheni zote za redio tanzania nzima pamoja na nje ya mipaka ya tanzania umesambazwa kwa ukaribu na kampuni hii ya skillman media na hivi karibuni utafanyiwa video ili mashabiki wapate kitu roho inapenda, vile vile tayari wimbo huo upo katika mitandao ukiwemo mtandao wa pambe za taarab.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni