TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 17 Oktoba 2017

MWINYIMKUU:- NI KWELI MAINA SI MKE WANGU, TUMEACHANA KWA TALAKA.

Na pambe za taarab.

Ama kweli mapenzi ni kiti cha basi, ukishuka anapanda na kukaa mwingine!, lile penzi lililokuwa likigeuzwa kama la mfano kwa wana ndoa vijana kwenye tasnia hii ya taarab nchini kati ya Mwinyimkuu na maina thadei limevunjika na sasa kila mmoja anaishi kivyake.

Akifanya mahojiano katika group la whatsap la pambe za taarab siku ya jumatatu iliyopita, mwinyimkuu alikili wazi kumuacha Maina kwa talaka moja na kusema kwa sasa kila mmoja na maisha yake, sipendi sana kuzungumzia matatizo ambayo yalitokea kwenye ndoa yetu mpaka kufikia kuvunjika sababu ni issue yetu binafsi ila kikubwa mashabiki jueni tu kuwa tumeachana kabisa!.

Unajua sisi sio wa kwanza kuachana ingawa inaonekana ni vijana wadogo sana, nimeishi na maina kama mke wangu kwa takribani miaka minne, nahisi palipofikia panatosha kila mmoja aangalie mustakabali wa maisha yake mbele kwa mbele. Kwa sasa nipo huku zanzibar katika bendi ya magereza ingawa sijaajiriwa bado, pia ninae mpenzi ambae nampenda sana anaitwa Husna Hassan chitoto ambae tunaimba pamoja hapa ila yeye ni askari. Mashabiki wangu wasubiri kazi yangu mpya nimefanya hapa ktk bendi ya magereza ambayo nitaitoa hivi karibuni ambayo itaambatana na video kabisa naomba sapoti zenu kama ambavyo mlikuwa mkinisapoti zamani alimaliza kwa kusema.

Mtandao huu unawaahidi tutamtafuta Maina nae kwa upande wake azungumzie hili la kuachana na mumewe analichukuliaje?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni