TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 19 Oktoba 2017

HALICHACHI CLASSIC KUISIMAMISHA MANZESE NA VITONGOJI VYAKE KWA UTAMBULISHO MAALUM LEO.

Na pambe za taarab.

Bendi inayokuja kwa kasi ya khali ya juu jijini dar es salaam kwa sasa halichachi classic modern taarab chini ya mkurugenzi Amour magulu siku ya leo alhamisi wanatarajia kufanya utambulisho rasmi wa bendi sambamba na maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ya mkurugenzi huyo.

Akizungumza na mtandao huu muimbaji wa kiume wa bendi hiyo Omary Sosha alisema maandalizi ya show hiyo tayari yameisha kamilika kwani vijana walikuwa kambini tokea alhamisi iliyopita, unajua jumapili tuliacha kufanya show pale friends corner kwasababu tulitaka wasanii wetu wapate muda mzuri wa kufanya maandalizi ya show hii. akiendelea kuzungumza Omary Sosha alisema tunaomba wadau, mashabiki na wapenzi kujitokeza kwa wingi kwani nawahakikishia hawatojuta kulipa pesa yao ya kiingilio ambapo mdau unatakiwa uchangie mlangoni 5000/= kwa mtu mmoja alimaliza kwa kusema.

Show hiyo ambayo inafanyika leo alhamisi friends corner manzese ndani ya bar mpya kuanzia saa mbili kamili usiku hadi majogoo!. Wadau tujitokeze kwa wingi kuwapa sapoti wana halichachi classic modern taarab.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni