Na pambe za taarab.
Muimbaji machachari Mariam mohamedy au ukipenda muite Mariam Bss amefunguka mbele ya mwandishi wa mtandao huu nakusema kwa sasa hana time na jahazi modern taarab isipokuwa ile haki yake ambayo ameitolea jasho anaitaka na kamwe hawezi kuwasamehe.
Akizungumza kwa kujiamini Mariam alisema, unajua sanaa ndio kazi yangu ambayo mimi mwenyewe nimeichagua naendesha familia yangu kwa kazi hii, sasa inapotokea mtu au kikundi cha watu wanataka kunidhurumu kiukweli siwezi kukaa kimya huo ndio msimamo wangu, sisi kama wasanii tumewavumilia sana viongozi wa jahazi tukijua bendi inajijenga lakini wamekuwa hawana kauli nzuri kwetu, wanarudharau mnoo mpaka kufikia kutuita sisi machokoraa huo sio udhalilishaji?.
Yaani haki yetu wasitupatie, matusi watutukane na bado majina ya kejeli watuite je ni haki?, mimi nasema sitaki tena kuimbia bendi hii maana viongozi wake wamekosa utu nacwala hawajui kanuni za uongozi zikoje! Mimi siburuzwi waendelee kuwaburuza hao hao wanaonyenyekea jina la jahazi kwa upande wangu mimi sio limbukeni wakutetemekea viongozi eti kisa jina la jahazi...bendi kaondoka nayo mzee yusuph mwenyewe waliobakia pale ni wajanja flani ambao wamekuwa wakitunyonya tu hamna maslahi yoyote. Mimi labda niweke msimamo wangu siyumbishwi na wala sibabaiki ninachotaka kikubwa ni haki yangu ambayo sikulipwa senti tano...kuanzia zile show tatu za mtwara na show zingine mbili tulizofanya morogoro sikulipwa nahitaji pesa zangu siwezi kuwasamehe sababu nimekauka koo kwa kuimba nahitaji jasho langu nipewe ndipo tumalizane vizuri alimaliza kwa kusema.
Mtandao huu ulimtafuta mkurugenzi wa jahazi modern taarab Hamisi boha Nakutaka kujua juu ya madai haya ya Mariam, kwanza alishtushwa na habari hizi na pili alisema kuwa wasanii wote walilipwa katika show hizo zote na viongozi hawadaiwi, katika show za mtwara zilikuwa tatu na tuliwalipa elfu ishirini na tano kila mmoja kwa kila show moja na zile show za morogoro zilikuwa mbili ambazo tuliwalipa elfu ishirini kwa kila show moja, sasa huyo Mariam anaposema anadai akwambie kama hakupewa pesa alikula nini katika mizunguko hiyo? alihoji mkurugenzi huyo.
Wiki mbili zilizopita wasanii watano wa jahazi modern taarab hawakwenda ktk show iliyofanyika ikweta grill mtoni kwa Azizi ally jambo lililotafsiliwa na viongozi wa bendi hiyo kuwa ni mgomo baridi ambao waliufanya wasanii hao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni