NA KAIS MUSSA KAIS.
Wasomaji wangu wa blog bora kabisa ya taarab nchini tanzania ubuyu wa taarab nawakaribisha kwa moyo mkunjufu katika sagment hii ya makala ya wiki nami kais mussa kais kama ilivyo ada!.
Lililo mezani leo hii ni kuhusu mchakato mzima wa kuanzisha chama cha muziki wa taarab nchini tanzania, ambalo naweza kusema kuwa wadau na viongozi wa bendi za taarab wameshindwa kabisa kuufufua umoja huu ambao hapo kabla uliasisiwa na wakongwe wetu akina mzee muchacho na wengineo, ni zaidi ya mara nne viongozi wa muziki huu wa taarab wameitana ili kuzungumza namna ya kuurejesha umoja huu lakini bila mafanikio.
Viongozi wa muziki huu wa taarab nchini wamekuwa wabinafsi na hawajali maslahi ya wengine hususani wasanii wao, nawapongeza Amin salmin na Siza mazongela ambao walijitahidi sana kufuatilia usajili wa zamani waliosajili wazee wetu na kuweza kupatiwa mpaka katiba ambayo wazee wetu waliiwakilisha pale Basata "nakala ya katiba hiyo ninayo" ili waweze kutengua baadhi ya vifungu ambavyo vilikuwa vimepitwa na wakati na kuweka vya kisasa ili kuendana na wakati.
Katika vikao vya kuijadili katiba hiyo ya zamani pale travetine magomeni viongozi wa bendi za taarab walipewa taarifa lakini hawakutokea kabisa, nakumbuka watu ambao tulikuwepo pale ni mimi mwenyewe, mkurugenzi wa kongamoyo taarab Iqubar, mkurugenzi wa T motto Amin salmin, mkurugenzi wa segere Siza mazongela pamoja na mdau mkubwa wa taarab nchini Emanuel kalugira, kwa mtazamo wa haraka haraka utagundua kulikuwa na mapungufu makubwa kwa baadhi ya bendi kukosekana katika kikao hicho pasipo sababu yoyote.
Huu ni udhaifu na ubinafsi uliopo kwa baadhi ya viongozi wa taarab nchini, mnataka kusema kuwa hamjui umuhimu wa kuwa na chama katika muziki huu wa taarab ama lah?, chama cha muziki wa taarab ni muhimu sana katika kutetea haki zenu, mfano sasa hivi vituo vya redio vimepelekewa barua na serikali ili kuanzia tarehe moja mwezi wa nne waanze kuwalipa kila wanapocheza nyimbo zenu, lakini taarifa zilizoufikia mtandao huu ni kwamba kuna baadhi ya redio zinataka kugoma kucheza nyimbo za taarab sababu wanasema hawana pesa za kuwalipa!, naamini katika hili viongozi wa taarab ndipo utakapowaona unafiki na ubinafsi wao! wapo ambao watasema hawataki kulipwa pesa yoyote na nyimbo zichezwe tu! na wapo ambao watajaribu kugomea hili japo ni wachache, hapa ndipo unapokuja umuhimu wa chama cha taarab tanzania!.
Chama kingekuwa hai utetezi ungepatikana na kila kitu kingekuwa sawa ila kwa vile viongozi wa taarab ni wabinafsi ndio maana sasa wanaburuzwa na wataendelea kuburuzwa sana huku haki zao zikipotea.
Ushauri wa mtandao huu ni kwamba tunashauri na kuomba baraza la sanaa tanzania kuingilia kati na kusimamia kuanzishwa kwa chama hiki cha taarab tanzania, na hii ni kwa faida ya wasanii husika maana wao ndio wavuja jasho wanaostahiki faida za chama hicho, lakini kwa nguvu ya viongozi imeshindikana kabisa!, Basata tunaomba hili mlipe kipaumbele na mlifanye kwa haraka ili pia kunusuru haki za wasanii wa taarab nchini, kwa leo ni hayo tu tukutane tena wiki ijayo...Ahsanteni!.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni