Na pambe za taarab.
Kuna ule msemo wa kiswahili usemao "fuatilia yangu ili uchelewe kufanya yako" naweza kusema wahenga "shikamoo". Hivi karibuni kuna mambo yanaendelea kimya kimya toka katika kambi hizi mbili za Jahazi modern taarab na Yah tmk modern taarab na wahusika wakuu wa issue hii ni baadhi ya viongozi wa bendi hizi mbili zinazofanya vizuri kwa sasa katika tasnia hii.
Habari za uhakika zilizofanyiwa ufukunyuku wa ndani zaidi na mwandishi wa habari hizi zinasema kuwa baada ya wasanii watano wa jahazi modern taarab kugomea show iliyofanyika siku ya jumamosi ndani ya ikweta grill na siku iliyofuata yaani jumapili kuonekana Mishi zelle katika jukwaa la Yah tmk huku jahazi wakifanya show travetine, hapo ndipo palipozuka sintofahamu toka kwa wadau na wapenzi wa bendi hizo mbili.
Hilo moja, lakini jambo la pili ni kwamba kuna taarifa za uhakika zaidi zinasema kwamba Yah tmk inaendelea kuibomoa Jahazi modern taarab kwani muimbaji wa kutegemewa wa bendi hiyo " jina kapuni" wameshafanya nae mazungumzo ya awali zaidi ya mara mbili na wameshaafikiana pindi kile kilichotakiwa na muimbaji huyo kikitekelezwa na uongozi wa Yah tmk basi atajiunga nao...hili litakuwa ni pigo kubwa sana kwa bendi hii ya jahazi endapo tu muimbaji huyo "jina tunalo" ataondoka jahazi na kujiunga na Yah tmk.
Unapokaa na viongozi wa Yah tmk na kuzungumza kuhusu bendi ya jahazi watakwambia hiyo bendi haina maisha muda wowote itakufa maana kwa sasa hawana muelekeo wowote wanaganga njaa tu lakini katika ushindani hawapo kabisaaa yaani ni bora uitaje wakaliwao modern taradance chini yake Thabit abdul...subiri tumchukue huyu tegemeo lao alafu utaona kama wataendelea alijigamba kiongozi wa Yah tmk.
Kwa upande wa viongozi wa Jahazi modern taarab wenyewe hawana mpango wa kuchukuwa muimbaji wowote tokea Yah tmk tokea lile vuguvugu la kumrudisha fatma mcharuko kuzimwa angani tena kimafia zaidi na viongozi wa yah tmk. Ila kikubwa ambacho wanazungumza kuhusu yah tmk ni hili jambo lao la kufanya show ambazo akina mama wanaingia bure bila kiingilio...Taarab inapendwa zaidi na akina mama alafu wao wanaingia akina mama bure huku ni kuchemka kwa wazi wazi kabisa! hapa wanafeli sana alisikika kiongozi mmoja akizungumza mbele ya mwandishi wa habari hizi, akiendelea alisema kwa sasa hatutokuwa tayari kufanya nao show ya pamoja sababu tunawapa kiki tu wakati uwezo wao upo chini sana, mpaka sasa wanaendelea kupiga nyimbo za jahazi wakati wana nyimbo zao huoni kuwa huo ni udhaifu walionao? alihoji kiongozi huyo jina kapuni.
Vita hii inanikumbusha enzi ile wakaliwao walipokuwa na bifu zito na mashauzi mpaka kupelekea Hashim said kutoka mashauzi na kujiunga na wakaliwao. Lakini cha ajabu ukiwakuta viongozi hawa wa jahazi modern taarab na yah tmk modern taarab yamekaa pamoja hutoamini haya niliyoyaandika...ndipo pale niliposema kuwa hawa jamaa wanachekeana kinafiki tu ila upendo miongoni mwao hakuna kabisa, hebu tusubili tuone mchezo huu wa kuigiza baina yao utaisha vipi?.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni