Na pambe za taarab.
Ukipata bahati ya kukutana ana kwa ana na Achun Baa mkurugenzi wa bendi ya gusagusa iliyo na maskani yake magomeni jijini dar es salaam unaweza kustaajabishwa kwa ukarimu mkubwa aliojaaliwa na mwenyezimungu, wasanii sambamba na wadau hupenda kumuita "zungu la roho" kwa ule ustaarabu anaouonyesha kwa watu.
Hassan farouk au ukipenda muite Achu Baa kwa sasa ndio roho ya bendi ya gusagusa na amekuwa akiwaongoza vyema wasanii wake pasipo manung'uniko yoyote toka kwao, chini ya Achun Baa gusagusa imeweza kusafiri nje ya nchi tena ulaya mara kadhaa wa kadhaa, gusagusa imekuwa ndio bendi ambayo inapiga show za harusi au sherehe mbalimbali za mastaa mfano Diamond platinum, wema sepetu, Hamisa mobeto na wengineo wakiwemo viongozi wa serikali. Ukaribu huu wote umeletwa na Achun Baa kwa wema na ukarimu wake ambao huwa anawaonyesha wadau na mashabiki wa bendi hii pendwa.
Kwa sasa gusagusa min bendi wanafanya show zao katika ukumbi wa Hugo uliopo kinondoni jijini dar es salaam mara mbili kwa wiki ijumaa na jumamosi kwa kiingilio cha shilingi 7000/= kwa mtu mmoja, watu wanaokuja katika show za bendi hii ya gusagusa naweza kusema ni " high classic" huwezi kuwaona katika show za bendi nyingine mfano yah tmk, mashauzi, jahazi, wakaliwao na nyenginezo hii ndio sifa na utofauti wa gusagusa min bendi na hizo zingine zinazopiga miondoko ya modern na taradance.
Kuongoza kitu chochote ni kipaji toka kwa mwenyezimungu na kiukweli wa dhati Achun Baa amepewa kipaji hicho na anakitumia vyema kabisa, uongozi wa mtandao huu wa pambe za taarab tunapenda kumpongeza Mr Achun kwa weredi wake katika kuhakikisha bendi yake ya gusagusa kwanza inakuwa tofauti na zingine na katika hilo amefanikiwa na pili kuhakikisha gusagusa inafika mbali zaidi kimafanikio kuanzia kwenye bendi mpaka wasanii mmoja mmoja, hongera sana Achun Baa hongera sana gusagusa min bendi mapambano yanaendelea!.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni