Na pambe za taarab.
Sura sio roho na sura surambi ni nyimbo mbili zilizotoka kwa kufuatana mmoja ukiimbwa na Isha mashauzi na mwingine ukiimbwa nae Salma double S mke wa Fikirini urembo mpiga gita la solo maarufu katika muziki huu wa taarab nchini.
Ujio wa Salma Mamaa double S na ule wimbo wake wa sura sio roho ulitetemesha anga la muziki huu wa taarab na kuanza kuhoji Salma Mamaa double S ni nani?, kiukweli wimbo wake ulifanya vizuri sana kipindi kile lakini cha kushangaza baada ya pale hatukumsikia tena Salma! kulikoni? umekwama wapi? maswali ni mengi sana toka kwa wadau, tumekuwa tukipokea simu kutoka kwa watu mbalimbali wakiuliza ukimya wa muimbaji huyu vipi kuna tatizo?.
Mtandao huu kwa kuthamini mchango wa muimbaji huyu ambae aliimba wimbo huo akiwa na bendi ya mumewe Fikirini urembo iitwayo bahari modern taarab ndipo tukaona itakuwa vyema kama tutamshitua kwa style hii ili huko alipo aweze kuchakalika maana wadau na wapenzi wa taarab wamemiss vitu vizuri toka kwake, popote ulipo Salma au yeyote atakae soma habari hii basi amfikishie habari kuwa watu wanataka vitu vitamu zaidi ya sura sio roho toka kwake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni