Na pambe za taarab.
Malkia wa mipasho nchini Tanzania bibie khadija omary kopa amezungumza na mtandao huu juu ya matarajio yake na bendi yake ya ogopa kopa classic ni nini wameplan kufanya katika kuhakikisha wanaendelea kubaki katika ramani ya muziki huu nchini.
Mwandishi wa habari hizi alitaka kujua toka kwa malkia huyo je kwa mwaka huu 2018 amepanga kufanya nini ndani ya bendi yake?, Malkia alianza kwa kusema kwanza kabisa mwaka huu naona unanipa matumaini makubwa sana maana kwa upande wa bendi yangu haujaanza vibaya tupo vyema na tunafanya show kadhaa wa kadhaa mpaka katika mialiko ya harusi mbalimbali tumeshapiga. Jambo kubwa la kimaendeleo nina matarajio ya kutoa wimbo wangu mpya usemao "wigi linawasha" chini ya utunzi wake mwanangu young hassan ally, vile vile waimbaji wangu wote watakuwa na nyimbo mpya ambazo tutazifanyia shooting kabisa alisema malkia huyo.
Akiendelea Bi khadija alisema mwaka huu 2018 hakuna kupoa tutahakikisha mashabiki wa ogopa kopa na watanzania kwa ujumla wanapata burudani ya nguvu tokea ogopa kopa classic bendi, nimekaa na kugundua udhaifu wa watu wa taarab upo wapi hivyo nataka kuirudisha taarab katika ile nafasi yake kama ilivyokuwa zamani. Jambo kubwa ambalo napenda kuwashauri watu wa taarab kwanza kabisa tupendane, tushirikiane pia tujenge utamaduni wa kuwa tunakutana mara kwa mara ili kubadilishana mawazo na kupeana mbinu zaidi za kuinua taarab ambayo inaonekana kupotea taratibu alimaliza kusema malkia huyo.
Kwa sasa ogopa kopa wapo katika mikakati ya kuanza kufanyia mazoezi nyimbo zao mpya kabisa ukiwemo wimbo wa wigi linawasha ambao utaimbwa na malkia huyo khadija omary kopa, sisi mtandao wa pambe za taarab tutaaendelea kuwaletea maendelea ya bendi hii kila wanalolifanya ili wadau na wapenzi muwe mnajua ogopa kopa ni nini wanafanya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni