Na pambe za taarab.
Wimbo mpya kabisa wa mwana dada Isha mashauzi "Queen of the best melodies" uitwao nibembeleze ambao umepigwa katika style ya afrobeat umeendelea kufanya vizuri kupitia vituo mbalimbali vya redio nchini tanzania na nchi za jirani.
Nibembeleze wimbo ambao umejaa ujumbe wa mapenzi umekuwa kipenzi cha wasikilizaji wengi na kikubwa ni kwajinsi Isha mashauzi alivyolalamika kwa hisia ndani ya wimbo huo, katika redio moja iitwayo sibuka fm 94.5 alisikika mama mmoja aliejitambulisha kama Mama Rachel ndani ya kipindi cha chaguo la msikilizaji akichagua wimbo huo na kushusha pongezi za nguvu kwa muimbaji wa wimbo huu Isha mashauzi akisifia jumbe nzuri iliyo ndani ya wimbo huo sambamba na melodies iliyotumika akasema pindi anapousikia wimbo huo hewani hata kama alikuwa anafanya kazi zake basi huacha kwanza mpaka uishe wimbo huo ndio anaweza kuendelea na shughuli zake.
Tathimini ndogo iliyofanywa na mtandao huu kwa siku chache tu tokea kutoka kwa wimbo huo inaonyesha kuwa wimbo huo umepata mapokeo makubwa sana toka kwa wadau na unaweza kumrudisha Isha mashauzi katika ile nafasi yake aliyokuwa nayo enzi zile za Acheni kuniandama!, wimbo huo bado haujatufikia mikononi mwetu lakini pindi utakapo tufikia basi bila hiyana tutauweka humu nanywi wasomaji wetu kuupakuwa au kuusikiliza, tunapenda kutoa pongezi za dhati kwa Isha mashauzi kwa kazi nzuri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni