Mwinjuma Muumini au kocha wa dunia kama ilivyozoeleka kwa wapenzi wake, ni msanii nguli wa muziki wa dansi japo kwa hivi karibuni amekuwa akionekana akiimba muziki wa taarab. Mtandao wa Ubuyuwataarabutz.blogspot.com uliamua kumtafuta Muumini ili aweke bayana kwa wapenzi wake kulikoni tena mbona amekuwa akionekana na huku upande wa pili?.

Akiendelea alisema, nilipokuja na wimbo wa kigodoro kimelowa maji watu walijua nimebeep tu, simu zikawa nyingi wakitaka kujua nini kinafuata baada ya pale?, sasa kupitia ubuyu wa taarabu naomba waelewe wazi kwamba sasa nimeamua kuja rasmi ktk taarabu na nakuja na wimbo uitwao JASHO LA BABA. huu ni wimbo mzuri zaidi ya ule wa kigodoro, wasubiri kupata vitu adimu sana toka kwa kocha wa dunia.
Nina mipango mingi sana ya maendeleo katika muziki huu wa taarabu hapa nchini lakini ni mapema mno siwezi kuanika hadharani
, ila wale waimbaji wakiume wa taarabu nchini tanzania wakae vizuri Muumini nakuja kiukweli ukweli kabisa. Ubuyuwataarabutz.blogspot.com tunasema karibu sana Muumini katika soko la ushindani wa muziki wetu wa taarabu nchini tanzania, kikubwa tunahitaji mabadiliko makubwa katika muziki huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni