TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 22 Oktoba 2014

SAKATA LA FUNGAKAZI MODERN TAARAB LAINGIA AWAMU YA PILI.


NA KAIS MUSSA KAIS
.


Kais Mussa Kais's photo. Bendi ya fungakazi modern taarab yenye maskani yake kigamboni jijini Dar, mwishoni mwa mwezi uliopita ilipatwa msukosuko wa kuondokewa na baadhi ya wasanii wake wa muhimu kwa sababu mbalimbali. Dawati la UBUYU WA TAARAB lilimtafuta temba ili athibitishe madai hayo, na alisema. Unajua ndugu ADMIN, kuondoka kwa wasanii wachache kati ya wasanii wengi tuliopo fungakazi ni kawaida ya wasanii na wala si jambo geni kwa msanii toka sehemu moja kwenda ingine, basi ndivyo ilivyo kwa wasanii hao ambao hawapo fungakazi kwa sasa.

Natambua wasanii wawili tu ndio waliotoka fungakazi nao ni Ashura Machupa na Senior Bachelor, ikumbukwe Ashura alihama tangu tarehe 6 kwa makosa mengi ya kinidhamu, kwa kulinda heshima ya uongozi na msanii siwezi kuyasema, lakini Senior pia ametoka bila ugomvi na ubishani wowote ameomba kujaribu maisha kwa upande mwingine.

Vile vile napenda kuchukuwa fursa hii kukanusha kuondoka kwa wasanii wangu wawili ambao ni Wahida Daddy alieimba Muungwana Haumbuki na Salma Mikausho alieimba Si bure una radhi ya mume, wote ninao katika bendi yangu ya fungakazi modern taarab. Nawapa pole wadau kwa kuongopewa, na kupewa taarifa zisizo za kweli. Fungakazi tunakuja kivingine, tuna nyimbo zifuatazo zipo jikoni zinaandaliwa, Jenereta bovu halina spea, Umekwama wapi na ingine inasema Walahi sikujibu. nyimbo hizo tatu zitathibitisha uwezo nilionao katka kutunga. mwisho napenda wadau wajue kwamba AUNT LATIPHA bado yupo na anaisapoti fungakazi kama kawaida.

Kais Mussa Kais's photo.
Dawati la UBUYU WA TAARAB lilimtafuta Senior Bachelor azungumzie hili nae alisema, Wahda Daddy ambae kwa sasa ana jina jipya la usanii la "Sumuni Salum Daddy" na Salma Mikausho wote ni wasanii wangu ndani ya Bongo Stars Modern Taarab na tayari wana nyimbo mpya kabisa, wimbo mpya wa Salma Mikausho unaitwa Funga Domo na ule wa Wahida au Sumuni Salum Daddy kwa sasa unaitwa Fisadi Kafilisika. ADMIN sikuishia hapo nilinyanyua simu yangu na kumpigia Salma Mikausho ambae alinithibitishia kuwa kwa sasa yeye ni msanii wa Bongo Stars modern Taarab na hayupo Fungakazi tena, nilipompigia Wahda Daddy simu yake haikupatikana hewani. Napenda niwaahidi wasomaji wangu kwamba nitamtafuta Wahda nae azungumzie hili kwa upande wake, wala msijali. HUU NDIO UBUYU WA TAARAB, UMEJAA VIUNGO TELEEEEEEEE!!!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni